Pata picha kwa miaka 17 Mama huyu Semeni Selemani hajaonana na Mtoto wake na amekua akimtafuta kila Kona bila mafanikio lakini leo amekutanishwa nae kupitia kipindi cha Redio cha LEO TENA Clouds FM
Semeni Selemani ambaye ni Mkazi wa Tabata DSM amesema alikua akiwatafuta Watoto wake wawili ambao walimpotezana kwa nyakati mbili tofauti ambapo wa kwanza ni huyu Mwita.
“Kutokana na ugumu wa maisha hatukuwa tunaishi pamoja na Baba yao, mimi nilikua naishi kwa Mama na yeye alikua anaishi kwa kaka yake, Baba yao alikuja na kusema anamuomba Mwita aende kupanda msalaba kwenye kaburi la Babu yake, baadae Baba yao akaja tena kumchukua Mtoto wa pili mimi sikuwepo nyumbani"
"Ikabidi niende Ilala alikokuwa anaishi Baba Mwita nilipofika wakaniambia Baba Mwita haishi tena hapa maisha ya mjini yamemshinda ameuza vyombo na kurudi Musoma, Watoto wote walitoroshwa kwangu na Baba yao wakiwa wadogo na sikuwaona toka hapo ndio juzi Mama yangu akaniambia huu ni mwaka wa mwisho lazima Watoto wangu niwaone twende CLOUDS kwenye kipindi cha LEO TENA ambacho huwakutanisha Wazazi na Watoto wao na leo ndio tumekutanishwa”
Mtoto wa pili wa Semeni aitwae Ngai ameshindwa kuja kuonana leo na Mama yake kutokana na mitihani aliyonayo shuleni ila Baba yao aitwae Adam pamoja na Mwita walifika CloudsFM leo na kukutana na Semeni baada ya miaka hiyo 17 ya kutoonana wala kuwasiliana.