Imeandikwa na @swalehmawele
FT: Yanga SC 0-0 Simba SC.
[emoji344] Ilikuwa ni mechi nzuri katika sanaa ya uzuiaji na haikuvutia kwa sababu hazikuonekana zikitengenezwa nafasi nyingi za kufunga, lilikuwa ni swala la nani angeweza kufanya kosa kubwa ili aadhibiwe, timu zote mbili zilikosa funguo ya kuifungua safu ya ulinzi ya timu pinzani ( unlock defensive patterns ).
[emoji344] Mohammed Nabi aliuweka mtego wake katika kipindi cha kwanza kwenye turn overs ( Simba wanapoupoteza mpira ), aliitaka timu yake iwe direct wanapoupokonya mpira, pasi tatu mpaka nne wawe kwenye zone ya Simba na watengeneze nafasi, tatizo lilikuja kwao katika uharaka wa wachezaji wa Simba kwenye kuziba mianya ( coverage ).
[emoji344] Simba ilichagua kucheza taratibu hasa kwenye eneo la kiungo, unaweza kucheza na Yanga kwa zaidi ya siku mbili na wasikupe mianya, mikimbio inayofanyika mbele ya safu ya ulinzi, unategemea nini dhidi ya quality kama ile? ndicho kile kilichotokea, mikimbio mbele ya safu yao ya ulinzi.
[emoji344] Kipindi cha pili walimu wote wawili walibadili game approach, Mohammed Nabi akaweka presha wakati ambao timu ina mpira au haina mpira na Pablo Franco akaziwinda pasi za kuchonga kutoka kwa Rally Bwalya zinazovuka safu ya kiungo ya Yanga baada ya kushindwa kwenye penetration passes, sub ya Bwalya ilikuwa ni ya kimkakati zaidi, pia haikufanikiwa kwa sababu Yanga walicheza aerial duels nyingi zaidi.
[emoji736] Inakera kucheza dhidi ya Kibwana Shomary, alicheza vyema mbele ya Morrison, akaonyesha umwamba kwa Sakho na hakumuhofia Shomary Kapombe.
[emoji736] Zipo nyakati ambazo ulikosekana ukomavu na uthubutu, wachezaji wengi walifikiria kwanza kuzisaidia timu zao zisifungwe, pakubwa ilipunguza ufanisi wao katika forward movement.
[emoji736] Henock Inonga [emoji119][emoji119] wow, anacheza kama hatacheza tena, mwanaume wa shoka mno, anacheza kwa ajili ya timu na mashabiki.
[emoji736] Aishi Manula na Djigui Diarra walikutana na mechi nyepesi kwa upande wao, hawakujaribiwa mara nyingi.