Makapuku Forum

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema ameziona video fupi kuhusu maduka ya dawa ambazo zinaonesha baadhi ya wauzaji wa dawa wakihojiwa kuhusu dawa na kuonesha kutokuwa na ujuzi wa kuzitambua dawa hizo kiundani.

Ummy amesema "Nawashukuru walioibua hili, ni kweli hii changamoto ipo, ninaliagiza Baraza la Pharmacy Tanzania kutimiza wajibu wao kikamilifu ikiwemo kuchukua hatua maramoja na kuhakikisha maduka ya dawa yanaendeshwa kwa mujibu wa sheria na kanuni"
 
Baada ya ile video iliyoonekana Mtandaoni ikimuoesha Kijana Mmachinga Tumain Saimoni Mkono akichukuliwa ndizi zake na Mgambo wa Hamshauri ya Jiji la Mwanza kitendo ambacho kimepelekea Serikali kuchukua hatua ya kuwafuta kazi Askari Mgambo waliohusika kwenye hilo tukio, Kijana huyo hakuwa amezungumza popote na leo @AyoTV_ imempata kwenye mahojiano.

“Namshukuru Rais Samia na Mkuu wa Mkoa, kwa namna nilivyo sikuwahi kuota ipo siku nitakaa na Viongozi, nimesikitika wamefukuzwa kazi ila nimewasamehe”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…