Makiwendo
JF-Expert Member
- Aug 12, 2015
- 10,031
- 34,666
Ahsante Auntie...Ngoja nimsome Mke wa ShaabanZamaradi mketema
KWA wanaotoa kejeli juu ya Mzee Mrema na kuuliza KWANINI ANAOA mnatakiwa kujua huyu ni mtu mzima sasa na hali yake inajulikan!! huenda watoto wote ni wakubwa na kila mtu yuko kwake, kwa hali yake anahitaji muangalizi wa karibu mno ambae sio wa kuja na kumuona tu ila wa kuwa pale muda wote, hata kama una pesa za kulipa wafanyakazi kuna vitu hutamani vionwe na wafanyakazi ila mtu wako wa karibu anaeweza kukufichia AIBU ZAKO!!!! na hakuna zaidi ya MKE!! sio mara zote watu huolea raha mara nyingine huoa kwa shida, japo sisemi kama kwa Mzee Mrema iko hivyo!!! Sasa kabla hamjaanza kutoa maneno yasiyofaa vaeni viatu vya mtu kwanza, tusipende kuhukumu situations ambazo hatujawahi kuziishi
Na zaidi nimpongeze huyo Dada kwa UBINAADAMU WAKE na mapenzi kwa Mzee wetu, lakini jambo moja ili ndani muwe na amani Ziba masikio, na huku mitandao pita kama kujifurahisha lakini usizingatie chochote, maisha yako yasiendeshwe na maoni ya watu ila UKWELI WA MAISHA YENU!!! Kwa ninachokiona kuna muda mitandao kama ilikuingia hivi na haya maneno ya wasema chochote yamekuchanganya na kukuvuruga ndiomana hauko huru na siku yako kubwa, lakini nikwambie tu SIO FEDHEHA na hakuna ulichokosea!! Hizi kejeli zisifanye uharibu kile ulichokubaliana nacho kwa roho moja, sababu zilizokufanya ukubaliane na uamuzi wa kuolewa mwanzo kabla Dunia haijajua ndio SAHIHI!!! Na haya maneno hayabadilishi usahihi wa sababu zako!! Wewe ndio UNAJUA MAISHA YAKO, umeamua kuolewa mwenyewe, na ndoa ni jambo la heri sio aibu, Olewa tu kwa amani na Furaha kipenzi, AMINI CHA KWAKO ILI WENGINE TUKIAMINI! Ukionesha wasiwasi watu wataanza kuwa na wasiwasi na maamuzi yako, usijikoseshe amani kwa mitandao, itasababisha kumkosesha hadi mzee amani ndani, kitu kidogo utakuwa unarudi kwa mzee matokeo itageuka manyanyaso, MPENDE MZEE, Muenzi, mpe faraja, mtoe upweke, Mlee, Mlinde, Muhudumie nina uhakika ndivyo anavyovihitaji kutoka kwako
Na sisi watu hebu tupunguze maneno, Kitanda usichokilalia hutojua kunguni wake, mwacheni mzee apate utulivu na Dada aishi maisha yake!!
NB:Nikupe moyo tu Dada kuwa Proud na mumeo, usione aibu,kuna wanawake huku KWETU Kinondoni wangepata hiyo nafasi ungechoka wewempende mzee wako View attachment 2163313

Naye ana magazeti jamani


mpende mzee wako

