CHAMBUA: MAYELE ABADILIKE ANAKOSA MABAO YA WAZI
.
Nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Sekilojo Chambua amesema licha ya Fiston Mayele
kuibeba Yanga lakini kitendo cha kukosa mabao ya wazi kinaweza kuigharimu timu hiyo katika mechi zijazo:
.
“Anaongoza kwa mabao kwenye ligi na hata timu yake ila ana udhaifu ya kushindwa kutumia nafasi nyingi anazozipata uwanjani, hivyo ni jambo analotakiwa kulifanyia kazi ili kuendelea kuibeba timu yake na kutimiza azima yao ya kutwaa ubingwa msimu huu.
.
“Anatakiwa kuongeza utulivu anapolifikia lango, azidishe umakini pindi anapopoteza nafasi lakini ajibidiishe zaidi na kudhihirisha ubora wake kwa kufunga mabao ya aina zote kwani kwani amekuwa akifunga mabao mepesi sana.”
.
WANANCHI mmemsikia Lijendi __!!