Makapuku Forum

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaziri ambapo kwenye Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amemteua Dr. Anjelina Mabula kuwa Waziri huku Naibu Waziri wake akiwa Ridhiwani Kikwete, hapo kabla Waziri alikua William Lukuvi.
 
Rais Samia amemuhamisha Waziri Innocent Bashungwa kutoka Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo na sasa atahamia Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
 
Rais Samia amemuhamisha Mohamedi Mchengelwa kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora amehamishiwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…