Makapuku Forum

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (Duwasa), Aron Joseph ametangaza dau la Sh100,000 kwa mtu atakayetoa taarifa sahihi zitakazosaidia kukamata wezi wa maji.

Joseph alitangaza dau hilo wakati wa kuhamasisha mkakati wa kudhibiti wizi na uvujaji wa maji katika mitandao ya Duwasa kutokana na kuwapo maeneo mengi yanayovujisha maji katika mkoa huo, huku mengine yanadaiwa kutobolewa na wananchi.
 
Shida ya usafiri kutoka mkoa wa Kilimanjaro kwenda Mkoa wa Arusha nyakati za jioni umefanya baadhi ya wasafirishaji kupandisha nauli kutoka Sh2,500 hadi Sh5,000.

Adha hiyo imesababishwa na uchache wa magari, hivyo kusababisha abiria kuwa wengi katika kituo cha mabasi cha Moshi Mjini.
 
Klabu ya Simba imewaacha wachezaji wawili katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili [Duncan Nyoni na Abdulsamad Kassim] wakati golikipa Jeremiah Kisubi akiwa ametolewa kwa mkopo kwenda Mtibwa Sugar.
 
Mshambuliaji wa Namungo FC Reliant Lusajo amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tamzania Bara kwa mwezi Disemba 2021.

Lusajo amewashinda Saido Ntibazonkiza wa Yanga na Haji Ugando wa Coastal Union ambao aliingianao kwenye fainali.
 
Melis Medo [Kocha wa Coastal Union] amechaguliwa kuwa kocha bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mwezi Disemba 2021.

Medo amewashinda Pablo Franco wa Simba na Nesreddine Nabi wa Yanga walioingia fainali. Mwezi Disemba Coastal Union ilishinda mechi tatu na kupoteza mchezo mmoja na kupanda toka nafasi ya tisa hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi.
 
"Mwandishi ameuliza kwamba kulikuwa na Sukuma Gang ambayo kazi yake ni kumuharibia Rais Samia Suluhu na unaniambia kuwa Mimi nasemwa kuwa ni Kiongozi wa Sukuma Gang sasa ndio nathibitisha hapa kwamba Mimi sio Kiongozi wa Sukuma Gang ndio maana namtetea Rais"

"Kuhusu hoja kwamba Ndugai ameomba msamaha na Mimi ni Kiongozi wa dini ambako ndiko msamaha unaishi kwanini nisimuombee msamaha, kanuni ya msamaha ukimsamehe Mtu sio lazima muwe wote mnaweza kusameheana na mkasema tumesameheana lakini tusiwe pamoja na hiyo ndio nashauri kwa Ndugai, msamaha umepokekelewa nahisi lakini namshauri asiwe pamoja na Mama Samia, ajiuzulu" ——— Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima.
 
Ukurasa wa Twitter wa Bunge la Tanzania umethibitisha kwamba Job Yustino Ndugai amejiuzulu nafasi ya Uspika katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo taarifa hiyo imesema "leo January 6 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa CCM kujiuzulu nafasi ya Spika, uamuzi huu ni binafsi na hiari na nimeufanya kwa kuzingatia na kujali maslahi mapana zaidi ya Taifa langu, Serikali na Chama changu cha CCM"
 
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amejiuzulu nafasi hiyo kuanzia leo Januari 6, 2022 kwa hiari yake mwenyewe kwa kulinda maslahi ya Taifa, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania (84) ibara ndogo ya 8 inaeleza kwamba, pindi kiti cha spika itakapokuwa wazi, hakuna shughuli yoyote itakayotekelezwa katika Bunge (isipokuwa uchaguzi wa Spika) wakati wowote ambao kiti cha Spika kitakuwa ki wazi.

Hii inamaanisha kwamba, ili shunguli za bunge linalotarajiwa kuanza Februari 1, 2022 ziweze kuendelea, ni lazima kwanza limchague Spika.

Kwa mujibu wa katiba, (84)(1), spika atachaguliwa na wabunge kutoka miongoni mwa watu ambao ni Wabunge au wenye sifa za kuwa Wabunge; atakuwa ndiye kiongozi wa Bunge na atawakilisha Bunge katika vyombo na vikao vingine vyote nje ya Bunge.
 
Albert Chalamila amesema hataki katiba mpya wala marekebisho yake. Ameeleza hayo akikanusha habari zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba anaunga mkono mabadiliko ya katiba.

"Wala sihitaji hiyo katiba mpya, wala sihitaji hayo marekebisho,"- amesema Chalamila.

Binadamuuuuu.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…