[emoji3578][emoji3578] Scandal24
FOOTBALL ECONOMY || BRANDING.
.
[emoji921]Sura ya nje ya Taasisi ni ishara ya namna Taasisi zinafanya kazi kutoka ndani. Namna Taasisi inavyozungumzwa ndivyo kwa asilimia kubwa inaathiri namna yake ya utendaji. Hivyo katika moja idara muhimu ni idara ya Mahusiano na Mawasiliano, mtu anayeteuliwa kuisemea Taasisi ni lazima awe mtu anayeenda mbele kuiheshimisha Taasisi.
.
[emoji921]Kuna kauli mbaya sana huwa naiongea, sio kama nawadharau watu hapana ila naongelea matokeo ya wao kuwa kwenye nafasi fulani. Football ya Tanzania imejaa MASELA katika kila Idara, uongozi, makocha na hata wanaozisemea klabu nyingi ni watu wa Hovyo na wanaongea hovyo hovyo wakifikiri ndio namna nzuri ya kuzisemea klabu zao.
.
[emoji921]Niliwahi kusema kua klabu ya Simba inapambana sana kuondoa picha ya USELA kwenye namna ya kuiongoza klabu yao. Simba imeamua kutengeneza Taasisi inayoheshimika na sio Taasisi inayosemeka sana, CREDIBILITY ndio kitu ambacho Simba imeamua kutengeneza na kiukweli inawasaidia sana kuifanya Simba ya kibiashara.
.
[emoji921]Hongera Simba kwa Kumpata Ahmed Ally na Hongera Ahmed unakwenda kufanya kazi na Taasisi ambayo inafanya TRANSFORMATION ya uendeshaji, wameona unafaa kuisemea Klabu yao na kuimbia DUNIA mazuri ya Simba.
.
NB:
Naamini sitosikia ahadi za kutembea UCHI mitaa ya Dar Es salaam.
.