

Farhan Jr
Napitia text ya Profesa hapa! Leo hajanipigia simu ila kaniachia texts tatu WhatsApp maana yupo busy na vikao huko Dodoma!
Prof anasema;

Mwanangu Farhan we all dream to have the team of the Drogbas! Kuna muda watoto wetu wanafanya kila kitu walicho nacho mguuni ila wenzetu kuna muda wanafanya kila kitu kilichopo kichwani
Prof anasema hata Misri walikuwa wanapata wakati mgumu kuelekea world Cup kwakuwa kuna muda hawakuwa na wachezaji wengi Ulaya, walicheza kwa tamaduni za Kiarabu tu ndio maana walitamba AFCON ila World Cup ilikuwa ndoto
Una Ivory Coast yenye wakina Drogba kibao wanatamba Ulaya, wanajua nini kinahitajika kwenye mechi za presha na mpira wa malengo kwakuwa wanapikwa hivyo na vichwa vyao vipo hivyo!
Taifa Stars ni timu nzuri na Vijana wana vipaji vikubwa sana ila wanapaswa kutoka wengi kwenda nje ili kuwa na kitu cha ziada kichwani, ijapo wamepambana sana! Ila still we need to have the team of Drogbas!

Kwenye umri wa miaka 20+ Tayari Kijana Feisal Salum anakuonesha ana kila kitu cha kuondoka ndani ya nchi na safari ya kwenda Magharibi, lakini nani anajali?
Huwezi kuwalaumu Yanga Afrika maana wamempa platform, huwezi kumlaumu Feisal maana tayari ameonesha, tulaumu Agencies za mpira na TFF ni muda wa kubadili set up na kuunda mahusiano mazuri na Kampuni za Mawakala na timu nje ya nchi, iwe rahisi kupata masoko ya vijana
Ifike wakati tuitazame Zanzibar kwa jicho la pili kama ambavyo Ujerumani iliitazama Ruhr Region (Ukanda wa viwanda) kwa jicho la pili, kwenye nchi lazima kuwe na sehemu moja ambayo ni kitovu cha vipaji, Zanzibar naiona hivyo

Kijana wangu nasikia kwenye harambee ilipatikana BILLION 1.6 Yes ndio pesa kama hiyo ipatikane nyingine wakajenge Academy Kigoma, Mwanza, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Zanzibar, Dar Es Salaam na Pemba
Nchi iwe na Technical centres zake na Academy zake atleast kila Kanda kuwe na Mkoa mmoja wa kimpira, UMISETTA ziwe Kikanda na vipaji vipelekwe maeneo husika, tuanzie chini kwenda juu! Inawezekana maana soka ni biashara kubwa tu