[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Suala la nembo ya Mdhamini ambaye ni NBC dhidi ya Yanga wala sio gumu na kubwa kama watu wanavyolichukulia, ni suala Jepesi sana linaongeleka
Yule Twiga wa NBC ni kweli ana rangi nyekundu ila Wananchi wana utamaduni wao ambao hautaki nyekundu kwenye jezi zao! Sasa Nilitaka kujua hili linaishi vipi??
Nikamtafuta Kaka yangu mmoja yupo kwenye Kampuni ya VODACOM kutaka kujua suala Lao na Yanga waliliendesha vipi na hatimae Wananchi kutumia rangi tofauti??
Kwanza kabisa yeye akaniambia hili suala ni mazungumzo kati ya Mdhamini na timu, hapa TFF na TPLB wao Kazi yao kusimamia kanuni ila wataheshimu makubaliano kati ya timu husika na Kampuni (Mutual agreements)
Hapo tu nikajua hii kumbe ni issue ya NBC na Wananchi kukaa round table kisha TPLB na TFF wao wataheshimu kile walichokubaliana kuhusu rangi, ila mpaka sasa TPLB wanasimama na makubaliano ya kimkataba kati yao na Mdhamini wao NBC
Turudi kwenye hoja ya msingi, Je VODACOM na Yanga walitatua vipi ilihali tunajua Voda wanatumia kidoa chekundu?? Kaka yangu akaanza kunipa Elimu kuhusu hilo
Akasema kuna kitu kinaitwa BRAND GUIDELINES! Hakuna Kampuni yenye rangi moja pekee, mfano Vodacom wana Nyekundu, Nyeusi na Nyeupe! Hizo ndio rangi zao ambazo zinaweza kutumika kwa mazingira tofauti
Akaniambia wala hapakuwa na shida kati ya Yanga na Vodacom kwakuwa GUIDELINES zipo na Yanga kwa tamaduni zao wakasema wataenda na doa jeusi kwenye jezi yao! Na hapo hapo akaniambia hadhani Kama kuna utata wowote kati ya Yanga na NBC, ni suala jepesi la kureview GUIDELINES tu
NBC wanaweza kuwa na rangi zaidi ya moja, watakaa mezani na kureview kwakuwa zipo rangi nyingi ili kuepusha mazingira Kama haya
Nami nikaenda beyond kwa issue kama ya PSG ambao kulinda tu utamaduni wao wa Mashabiki kuchoma moto uwanjani, basi wanalipa faini ya Dola elfu 30 kila msimu, kulinda tu utamaduni wao wa moto! Ina mantiki kibiashara na kiutamaduni
Jambo jepesi tu