[emoji3578][emoji3578] Kelvin Rabson
Moja ya mchezo bora sana usiku wa leo pale Italy...Atalanta wakionesha uwezo mkubwa sana[emoji91]... lakini alikuwa ni Cristiano alie simamisha furaha yao.
Man United wanakuwa wazi sana bila mpira, kuanzia eneo la kiungo mpaka ulinzi, hawaweki presha kwa mpinzani, hawaweki presha kwenye mpira....yaani mpaka unajiuliza ma boss wa United wanaangalia mpira na wanaona haya matatizo.
.
Atalanta kila wakihamisha mpira kutoka upande mmoja kwenda mwingine inakuwa matatizo kwa United...walitumia mabeki watatu sawa na Man United lakini pressing yao ilikuwa bora sana, hawakuwaruhusu wachezaji wa United kuchezea mpira mda mrefu.
.
Zapata...Ilićić....Paśaliç walifanya mikimbio sahihi na hatari nyuma ya safu ya kiungo ya United...tafuta nafasi, pasi kwa haraka..tanua uwanja zaidi...shinda mipira ya pili [emoji460]baina ya safu ya kiungo na ulinzi ya United kunao nafasi hiyo ndio waliotumia.
.
Man United bado wanao makosa mengi hasa wakati wa kuzuia Maguire asee unadhani amekuja bure...one vs one anapitwa bado anafanya uzembe kwenye kushinda mipira ya pili...hili litazidi kuwagarimu sana United....Baily ametuokoa sana.[emoji119]
.
NOTE:[emoji3578]Cristiano Ronaldo....Mr Uefa Champions League [emoji119] mechi 4 za UEFA zote kafunga....kaisaidia United wasipoteze poimts zote Form is temporary but class is permanent [emoji847]
.
Daah United itatuuwa kwa presha sasa[emoji23]
.
FT: Atalanta 2-2 Man United.