[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
Katika historia ya klabu zote kubwa duniani ukishafika juu all the way is down, ni kawaida kurudi chini na kuanza upya
Barcelona waliwahi kuanguka huko 1988 kwenye kile kisa maarufu cha Hesperia Mutiny, wachezaji na Viongozi walipishana sana ila wakarudi tena kwa nguvu
Ni kawaida kuanguka na kurudi tena Kama ambavyo Rais Perez wa Real Madrid alijiuzulu hata Ramon Calderon alijiuzulu ila Madrid ikarejea tena
Sikilizeni Simba, mpira ndivyo ulivyo hakuna asiepoteza na hakuna asiyejua Maana ya ushindani ila huu ni mpira wa miguu ni kawaida kutokea yanayotokea
Kwa Viongozi kama kuna Mtu anataka kubaki basi abaki na Kama mtu anataka kuondoka basi aondoke, huu sio muda wa kuwa wa Uvugu uvugu bali Kama moto uwe moto na baridi uwe baridi, Simba inahitaji sana mshikamano
Kwa bench la Ufundi, ni vyema mtambue hii ni Simba, ni klabu kubwa yenye malengo makubwa! Hizi kelele ni kawaida inaonesha ukubwa wa timu, endeleeni kufanya Kazi yenu mpaka itakapokuwa vinginevyo, mnafahamu kanuni za ajira ni kuajiriwa na kufukuzwa, mnafahamu basi msikate Tamaa fanyeni Kazi
Kwa Wachezaji, ninyi ni washindi tena wakubwa! Misimu minne mfululizo kwenye ubora kwa klabu na taifa lenu, hakuna anaewachukia, kikubwa ni kuendelea kupambania badge na watu watakumbuka daima majina yenu
Mimi Nipo upande wenu, sidhani Kama mnaenda uwanjani ili mpoteze wakati hii ni ajira yenu, endeleeni kupambana ni morali ile ile GO HARD OR GO HOME, kilichotokea ni mpira wa miguu, enndeleeni kupambana
Kwa Mashabiki wa Simba, huu ni mpira na hii ni timu! Msipende kupelekwa na upepo! Kama umeipenda timu kisa mtu basi jua mtu anaweza kuondoka ila Simba itasalia, timiza wajibu wako wa kikanuni ni kushangilia au kuzomea ila sio kupelekwa na upepo wa mtu
Hizi ni nyakati za kawaida tu kwenye mpira, kwanini muumie sana?! Kwanini mnahangaika kutaka kutakasa kaniki wakati ni rangi yake?? Hii ni Simba ni zaidi ya klabu, RESPECT [emoji110]