Nabi afichua siri ya Kiwango Bora cha Feisal Salum Feitoto:
.
“Hamjui kwanini amekuwa bora (Fei Toto) nilipoanza msimu nilikaa naye nikamwambia nataka awe bora msimu huu nitakuwa nampanga namba 10, akiwa hapo awe anarudi kukaba pale kati kazi ambayo anaifanya, pia awe akichezesha timu vizuri,” aesema Nabi na kuongeza;
.
“Majukumu hayo anayafanya vizuri sababu ni kijana mdogo ambaye ana nguvu ya kujituma lakini pia nikamwambia kufanya hayo pekee haitoshi, nataka pia afunge mabao kwa mashuti. Najua ubora wa Feisal anajua sana kupiga mashuti makali, ila nilimwambia nataka mashuti yanayolenga lango akiweza afunge, naona sasa ameanza kufanya kile ninachotaka.”
.
“Najua yapo mashuti yatakosa kulenga lango, ila yale yatakayopanguliwa na makipa, najua kuna Mayele. Huyu ni mshambuliaji anayejua kukaa maeneo sahihi sioni kama atakosa kumalizia nyavuni na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri,”