[emoji3578][emoji3578] Farhan Jr
YUSUPH ATHUMAN NA MAKAMBO, SIMULIZI YA MWALIMU NA MWANAFUNZI
Wakati nyasi za Allianz Arena pale Munich zinafuka moshi ya ukungu wa baridi kali sana, ni fainali ya UEFA hiyo ni Chelsea hao dhidi ya Bayern Munich ilikuwa 2012
Kinda Ryan Bertrand alionekana kama anapitia magumu eneo la kushoto, akatoka Frank Lampard mchezaji Mwandamizi akamuuliza Bertrand! "Kijana hii ni nini?" Ryan akajibu hii ni fainali ya UEFA
Lampard akamwambia "play the game not the ocassion" akimsihi asahau kuwa ni fainali ya UEFA, acheze kama mechi zingine, baada ya hapo Ryan alikuwa bora sana baada ya Legend kusema nae
Wakati Ronaldo anapitia magumu sana ilikuwa United vs AC Milan 2005 hiyo! Ronaldo anakula viatu kutoka kwa Gatusso mpaka anapanic! Ndipo Keane alimpa ule msemo maarufu zaidi England
Keane alimfuata Ronaldo na kumwambia "This is football Kid, either go hard or go home" alimwambia akomae ama aende nyumbani, Magwiji wana namna yao ya kuwaelekeza vijana wadogo kwenye soka
Nikurejeshe mpaka nchini Tanzania kwenye stori ya Kinda Yusuph Athuman na Heritier Makambo siku moja pale Avic Town Kigamboni kwenye mazoezi ya kila siku
Wakati Makambo na Yusuph wapo timu moja, zikipigwa ndefu Yusuph anacontrol anamsubiri Makambo kwenye njia anamuwekea kisha Makambo anaweka, hii ilijirudia kama mara nne hivi
Makambo akamuita Yusuph akamwambia njoo ucheze napocheza kisha niende unapocheza! Ulipigwa mpira mrefu, Makambo akaucontrol, on space yupo Yusuph, Makambo akaweka kambani mwenyewe
Kisha akamuita Yusuph kama Mdogo wake na kumwambia "Mdogo wangu napenda kitu chako cha kwanza cha kuichezesha timu, nataka pia uwe imara zaidi na zaidi kwenye hiki cha pili, nifuate"
Yusuph anapokea darasa zuri sana kutoka kwa Mayele na Makambo, wanampenda kama Mdogo wao na wanafanya kazi kama Kaka zake, hii ni faida kwa Yanga na Taifa letu