Yanga inajipanga na mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali wakikutana na Rivers United ya Nigeria na uhakika pale makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) upande wa Idara ya Mashindano yamefika majina 28 tu,
Orodha ya uhakika ambayo Mwanaspoti imeipata ni kwamba jina la mwisho kukamilishwa katika usajili huo ni kiungo Khalid Aucho ambaye Waarabu wa Lel Makkasa inayoshiriki Ligi Kuu Misri walikuwa wanadengua kutoa uhamisho wake wa kimataifa lakini baadaye wakaachia wenyewe.
Orodha ambayo Yanga imewasilisha inawajumuisha makipa 3 ambao ni Diarra Djigui, Erick Johola na Ramadhan Kabwili huku mabeki wakiwa 9 ambao ni Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Yannick Bangala, Dickson Job, Bakari Mwammnyeto.
Wengine ni Kibwana Shomari, Djuma Shaban, David Bryson, Adeyun Saleh na Paul Godfrey ‘Boxer’ watakaosimamia uimara wa Yanga katika safu ya ulinzi ya timu hiyo.
Yanga imewajumuisha viungo 6 ambao Mukoko Tonombe, Aucho, Feisal Salum, Zawadi Mauya, Deus Kaseke, Jesus Muloko, Farid Mussa, huku kwenye eneo la ushambuliaji itakuwa na watu 5 ambao ni Fiston Mayele, Heritier Makambo, Yacouba Songne, Said Ntibazonkiza na Yusuf Athuman.