Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata na linawashikilia Watu sita kwa tuhuma za kuwashambulia na kuwarekodi video za utupu Watu wawili Mwanaume (Rashid Kawanje) na Mwanamke (Anitha Laurian) na kuzituma mitandaoni wakidai kuwa wamewafumania.
Watuhumiwa hao ni Singiba Buchadi(42), Fundi umeme, Mkazi wa Kongowe mwisho,Dephina Buchadi (42), Mfanyabiashara, Mkazi wa Kongowe, Doratea Mathayo (39), Mkazi wa Kongowe Mwisho, Wilbard Teobard (55), Albert Buchadi (30), na Valenzi Silvester (40).
“Vitendo vya kikatili walivyovifanya Watuhumiwa hao ni pamoja na kutoa adhabu wakati wao si Mahakimu au Majaji, vitendo hivyo havikubaliki kisheria katika Nchi inayofuata mfumo wa utawala wa sheria na kwa sababu hizo watafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo”———-Muliro Jumanne , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM
Video nzima ya tukio hilo la madai ya fumanizi ipo kwenye Youtube ya ‘millardayo’ au bonyeza link kwenye Bio hapo juu kuitazama direct.