“Tumekuwa na mazungumzo mazuri na yenye kuamsha matarajio makubwa sana kwa Nchi zetu mbili, kwa yale tuliyotofautiana hayakuwa na misingi ila tu ni mitazamo tofauti ya Watu, uchungu wowote uliojitokeza ulikuwa uchungu wa uzazi na sio wa maradhi”———Rais Samia Bungeni Kenya
“Uchungu wa uzazi unaishia kuleta Mtoto na unaleta furaha kwenye Familia lakini uchungu wa maradhi unaishia kwenye kifo, sisi (Tanzania na Kenya) tunapokerana huo ni uchungu wa uzazi, tukae tuzungumze tupate Mtoto Amani tuendelee na uhusiano wetu”———Rais Samia
“Chini ya uongozi wangu, tutafanya kila tunachoweza ili kuimarisha uhusiano wetu, Dira ya Serikali yangu ni kudumisha ya awamu iliyopita na kuendeleza mapya, kama kuna ambalo linalega au uhusiano wetu unasuasua nimekuja kuyanyoosha yale yaliyojipindapinda”———Rais Samia
“Kenya ndio Nchi ya kwanza kwa mimi kufanya ziara rasmi, nilienda Uganda kusaini mkataba ila haikuwa ziara rasmi, ziara yangu ya kwanza rasmi tangu kushika Uongozi nimeanzia Kenya na sio kwasababu ni karibu kijiografia ila ni kwasababu ya umuhimu wa Kenya kwa Tanzania”———Rais Samia