BINADAMU MWENYE SURA MBILI
Edward Mordrake ni Mwingereza aliyezaliwa mwaka 1887 akiwa na sura mbili, moja ikiwa kwenye uso wake wa kawaida na nyingine nyuma ya uso (kwenye kisogo).
Inasemekana kuwa sura yake ya kisogoni haikuweza kula wala kuongea chochote na hata ikijaribu kuongea maneno yalikuwa hayasikiki lakini iliweza kulia, kucheka na kusikia kila neno.
Sura yake ya mbele ya uso imeelezwa kuwa ilikuwa ni nzuri na ya kuvutia (handsome face). Watu waliomuona na kuzungumza naye, wanamsifu Mordrake kwa uzuri wa sura yake ya usoni na tabasamu lake, lakini balaa lipo kwenye sura yake ya kisogoni ambayo ni ya kutisha na kuzeeka mithili ya kikongwe.
Wafanyakazi wa nyumba alimokua anaishi Mordrake walitoa simulizi kwa siri, ambapo walieleza hali ya maisha ya huzuni ya kijana huyo iliyosababishwa na miujiza na mabalaa yaliyoletwa na sura yake ya kisogoni.
Alijaribu kuwaomba madaktari wamfanyie upasuaji wa kuing’oa sura hiyo ya kishetani, lakini sababu za kitabibu zilizoonesha uwezekano wa yeye kupoteza uhai endapo atafanyiwa upasuaji huo, hivyo walikataa kufanya hivyo.
Mwaka 1910 akiwa na umri wa miaka 23, aliaamua kujiua kwa kunywa sumu baada ya kuchoshwa na mikasa hiyo ya sura mbaya aliyoiita kuwa ni ya kishetani.
Kutokana na hadhi ya ukoo wa Mordrake nchini Uingereza, historia ya maisha yake haikuweza kuwekwa wazi ili watu wengine wakajua maisha yake.