UNAAMBIWA Mwanaume mmoja nchini Japan akiwa na umri wa miaka 60 aliishtaki Mahakamani Hospitali moja ya Tokyo baada ya kubaini kuwa wakati anazaliwa Wauguzi walijichanganya na kumkabidhi kwa Mama ambaye hakumzaa March 1953 ambapo walimchanganya na Mtoto mwenzake aliyezaliwa dakika 13 baada ya yeye.
Mwanaume huyo alilalamika kuwa kujichanganya huko kumemfanya alelewe maisha ya kimasikini na single Mother wakati Mtoto mwenzake akilelewa Maisha ya kishua na Wazazi Matajiri———“Mwenzangu anamiliki Viwanda wakati waliompa ni Wazazi wangu, Mama yake ni huyu aliyenilea Mimi kimasikini”
Mahakama ya Wilaya Tokyo iliamuru Hospitali hiyo imlipe fidia ya Euro 227,000 (Tsh. Milioni 634) kwa makosa hayo ya waliyofanya huku wakimtaka Mwanaume huyo ikiwezekana akutane na Wazazi wake wa kweli ili wayamalize na kuishi pamoja.
View attachment 1765713