Makapuku Forum

“Nakwenda kufanya mabadiliko makubwa ya Mainjinia wa Maji huko Mikoani, pesa nyingi zinatoka Wizarani kwenda Mikoani lakini Mikoani kunasuasusa maji hayapatikani, wanaoshindwa kutupa maji wapishe tuingize damu mpya”———Rais Samia Suluhu Bungeni leo
 
“Tunakusudia kuelekeza nguvu kubwa katika ukuzaji wa Uchumi, Taifa letu limepata mafanikio makubwa kiuchumi katika miaka 5 iliyopita, Takwimu zinaonesha kwa Tanzania Uchumi wetu tumeusimamia kwa wastani wa 6.9% na kudhibiti Mfumuko wa Bei kwa 4.4%”———Rais Samia

“Takwimu zinaonesha Uchumi wa Nchi nyingi Duniani umeathiriwa na Corona, Tanzania nayo imeathirika kwa kushuka kwa Uchumi kutoka wastani wa 6.9% hadi 4.7%, Wataalamu wa Uchumi wanatuambia ili kuondoa umasikini Uchumi unatakiwa kukua angalau kwa wastani wa 8% kwa mwaka”———Rais Samia akihutubia Bungeni Dodoma leo
 
“Waziri wa Maji (Aweso) ile kauli yako unayowaambia wenzio ambayo nami niliikopa kwako ya ‘ukinizingua tutazinguana’ inarudi kwako, tunakwenda kuboresha upelekaji wa maji kwa Wananchi kwa haraka na tukishindwa Waziri wa Maji kabla ya kusema Mimi itabidi uondoke”———Rais Samia Suluhu Bungeni Dodoma leo
 
“Tutakuza usawa wa kijinsia kwa kuteua Wanawake wengi zaidi kwenye nafasi za Uongozi lakini kama nilivyosema ni kuendana na sifa na vigezo”———Rais Samia Bungeni Dodoma leo

“Mashirika mengi ya Umma yanaendeshwa kwa kusuasua, ikifika wakati wa kutoa gawio Serikalini Viongozi wa Mashirika hayo wanahangaika kutafuta gawio wakihofia nafasi zao, tutaboresha Mashirika ya Umma ili yawe na tija na kuzalisha faida”———Rais Samia
 
Hizi ni baadhi ya picha kutoka Bungeni Dodoma leo wakati wa Rais Samia Suluhu Hassan alipotoa hotuba kwa Bunge na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na mambo mengine Rais Samia amesisitiza kuhusu uwekezaji ambapo amesema———“Tutarudisha imani ya Wawekezaji na kutoa vivutio kwa Wawekezaji, tunalalamikiwa sana, kumekuwa na mchakato mrefu Watu wanapotaka kuwekeza Tanzania, Serikali ya Awamu ya Sita tunakwenda kukomesha hili na Uwekezaji utakwenda kwa haraka”

“Tutahakikisha tunaboresha sheria na sera zinazoleta vikwazo katika uwekezaji Tanzania, tutachukua hatua madhubutu kuboresha mazingira ya biashara, kutoa vivutio kwa Wawekezaji ili uwekezaji ufanyike kwa haraka”———Rais Samia
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…