Makapuku Forum

“March 23,2021 mwili wa Hayati Magufuli utaagwa Mwanza na baadaye kusafirishwa kuelekea Chato, March 24,2021 Wanafamilia na Wananchi wa Chato na maeneno jirani watauaga mwili wa Hayati Dkt.John Pombe Magufuli”- Rais Samia Suluhu
RIPHayatiMagufuli
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa shughuli za mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli zitafanyika Chato March 25, 2021 na kusema siku hiyo itakuwa ni siku ya mapumziko.
RIPHayatiMagufuli
 
“Leo sio siku nzuri sana kwangu ya kuhutubia Taifa maana nina vidonda vikubwa moyoni, kiapo nilichokula leo ni tofauti na vyote nilivyowahi kula katika maisha yangu, nimekula kiapo cha juu kabisa Tanzania nikiwa na majonzi tele, mniwie radhi nitaongea kwa uchache”-Rais Samia Suluhu baada ya kula kiapo

RIPHayatiMagufuli
 
“Natoa salamu za rambirambi kwa Watanzania wote kwa pigo hili kubwa ni msiba mzito ambao hatukuutarajia, sote tunafahamu namna Rais Magufuli alivyoipenda Nchi hii na alivyojitoa kuwatumikia Watu wake,ameibadili taswira ya Nchi kwa vitendo huku muda wote akimtanguliza Mungu”-Rais Samia Suluhu baada ya kiapo

“Dkt.Magufuli alikuwa Kiongozi asiyechoka kufundisha, amenifundisha mengi, amenilea na kuniandaa vya kutosha, tumepoteza Kiongozi shupavu, madhubuti, mzalendo, mpenda maendeleo na Mwanamapinduzi ya kweli”- Rais Samia

RIPHayatiMagufuli
 
“Nawashukuru CCM kwakuwa karibu nami tangu tulipopata msiba, nawashukuru pia Viongozi wa Vyama vya Upinzani kwa wingi wa salamu za rambirambi na kunipa pole tangu nilipotangaza msiba huu mkubwa, huu ni wakati wa kuzika tofauti zetu na kuwa wamoja kama Taifa”- Rais Samia Suluhu

RIPHayatiMagufuli
 
Hizi ni picha kutoka Ikulu, Dar es salaam leo wakati Samia Suluhu Hassan akiapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof.Ibrahim Juma.
 
“Huu ni wakati wa kufarijiana, kuoneshana Upendo, Udugu wetu, kudumisha amani yetu, huu sio wakati wa kutazama yaliyopita bali kutazama yajayo, huu sio wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele, ni wakati wa kufutana machozi”- Rais Samia Suluhu

RIPHayatiMagufuli
 
PICHA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri leo March 19, 2021 Ikulu jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuapishwa kuwa Rais.
 
PICHA: Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiongoza kuomba dua alipokwenda kumpa pole Mama Janeth Magufuli mara tu baada ya kuapa Ikulu jijini Dar es salaam leo March 19, 2021, pamoja nae ni Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Bashiru Ally na Binti wa Marehemu Rais Magufuli.

RIPHayatiMagufuli
 
Msemaji Mkuu wa Serikali Dr.Hassan Abbas ametangaza kuwa shughuli za mazishi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli zitafanyika Chato March 26, 2021 badala ya March 25,2021 ambayo ilikuwa imetangazwa awali, hii ni baada ya Zanzibar kuongezwa kwenye ratiba ya kuuaga mwili March 23,2021.

Kutokana na mabadiliko ya ratiba, sasa Dar es salaam mwili utaagwa March 20 na March 21,2021, kisha Dodoma March 22,2021, Zanzibar March 23,2021, Mwanza March 24,2021, Wanafamilia na Wananchi wa Chato wataaga mwili March 25,2021 na shughuli za mazishi zitafanyika March 26,2021.

RIPHayatiMagufuli
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge ametoa ratiba na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli ambapo Mkoa wa Dar es salaam umepewa siku mbili za kutoa heshima za mwisho.

Akitoa ratiba hiyo RC Kunenge amesema kesho Jumamosi March 20 kuanzia saa 1:00 -3:00 asubuhi itafanyika Misa takatifu Kanisa Katoliki Mt. Petro, saa 3:00 - 3:30 asubuhi, mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, saa 3:30 - 4:30 asubuhi itafanyika Misa takatifu ambapo saa 4:30 asubuhi hadi saa 9: 30 alasiri Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa, Wafanyakazi na Taasisi za Umma watatoa heshima za mwisho na saa 9:30 - 12:00 Wananchi watatoa heshima za mwisho.

Kunenge amesema Jumapili saa 2:00 asubuhi mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni Wananchi watatoa heshima za mwisho ambapo saa 10:30 Jioni hadi saa 11:00 jioni mwili utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo saa 11:00 jioni hadi Saa 11:45 jioni Mwili utasaririshwa kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma.

RIPHayatiMagufuli
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya maombolezo kufuatia Kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika Viwanja vya Kareemjee Dar es salaam leo.
 
“Nimepata tabu kuandika kwa kifupi kuelezea simanzi na masikitiko yangu kwa msiba mkubwa ulioukumba nchi yetu kwa kuondokewa na mpendwa wetu Mheshimiwa Rais Magufuli, nimelazimika kuyaambatisha hapa chini, Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema, peponi” ——— Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, swipe left kusoma yote aliyoandika Mstaafu Kikwete.

RIPRaisMagufuli #PumzikaBaba
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…