Makapuku Forum

Raia wa Kenya David Karega amehukumiwa kifungo cha miaka 100 Gerezani kwa kosa la kuwanajisi Watoto watano kwenye Kaunti ya Nakuru.

Amehukumiwa kwa kuwanajisi Watoto wa Kike watano wenye umri wa kati ya miaka 5 hadi 7 na kuwapa kila mmoja Ksh 10 (Tsh. 210) huku akiwatishia kutosema alichowafanya.
 
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imetajwa kuwa Hifadhi bora zaidi Duniani na kushika namba moja katika Hifadhi 25 zilizotajwa na mtandao maarufu wa Trip Advisor huku Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Tarangire zikifuatia katika ubora huo na kufanya Hifadhi za Taifa tatu kutoka Tanzania kuingia katika tuzo hizo kwa mwaka 2021.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro mbele ya Wanahabari Mkoani Morogoro wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Safia Jongo amesema Mama mmoja akiwa na Watoto wake wawili porini, ameng’atwa na nyoka aina ya Koboko na kufariki Dunia na kisha baadaye mwili wake ukaliwa na fisi.

“Mtoto wake mmoja pia na yeye aling’atwa na nyoka na kufariki kama ilivyomtokea Mama yake na akaliwa pia na fisi lakini cha ajabu Mtoto mdogo aliyekuwa mgongoni hakuguswa na nyoka wala fisi na alikaa porini kwa siku sita, na mpaka leo yuko salama baada ya kutolewa porini”- RPC Tabora

RPC Jongo amesema tukio jingine kutoka Tabora ni la Mtoto wa miaka saba ambaye ameliwa na fisi baada ya kuagizwa dukani usiku na Mama yake Mzazi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…