Shirika la umeme la Kenya, KPLC limelazimika kubadili mfumo wa nyaya za umeme zinazopita katika hifadhi ya wanyama ya Soysambu Nakuru, baada ya twiga wawili kufa baada kugusa nyaya hizo.
•
Shirika la wanyama pori la Kenya KWS lilijulishwa kuhusu vifo vya twiga hao adimu wa spishi ya Rothschild waliofariki kwa kupigwa na moto mkubwa hiyo jana 21 Februari.
•
Ripoti za awali zilisema twiga hao wamekuwa warefu na kumefika kimo cha nyaya za umeme Lakini wanaharakati wa mazingira wanadai nyaya za umeme ziliwekwa kwenye kimo cha chini kuliko ilivyokawaida na hivyo kusababisha ajali hiyo.
•
"Nyaya hizi za umeme zimekuwa zikiwaua twiga na wanyama wengine. Ripoti ya kiufundi ya kutathmini manufaa na hatari kabla ya mradi kuidhinishwa na serikali zinafanywa kiholela.
Inasikitisha kwamba hadi hali kama hii itokee ndio hatua ichukuliwe!"
Mwanaharakati mhifadhi wa wanyama Paula Kahumbu aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter .
•
Sasa KPLC wametuma vikosi vya wahandisi kusuluhisha tatizo hilo