Dondoo na tetesi za usajili majira ya kiangazi;
Clabu ya NCCR Mageuzi huenda ikaimarisha safu yake ya ushambuliaji kwa kumsajili winga wa CHADEMA ,Saed Kubenea hiyo kesho. (Nipashe)
Kiungo wa NCCR Mageuzi anayekipiga kwa mkopo CHADEMA , Anthony Komu amesema kuwa tayari amejiandaa na msimu ujao. (Jamvi la habari )
Mlinzi wa kati wa CHADEMA, Ester Bulaya amesema kuwa hana mpango wa kurejea clabu yake ya zamani ya CCM kwani ana uhakika na namba. (The Citizen)
Kiungo wa CHADEMA Peter Msigwa, anausishwa na vilabu kadhaa vya ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi na CUF (Majira)
Jeremia Maganja ambaye ameachana na miamba ya ACT Wazalendo, anasemekana kukaribia kusaini dili la.miaka 5 kukipiga CCM (Mwanahalisi on line)
Kinda wa CHADEMA Godlisten Malisa, amesema kuwa wazee kadhaa wamemfuata kuwania namba ya jimbola moshi vijijini (Tanzania Daima)
Wakala wa Steven Wasira amesema kwamba Esther Bulaya sio tishio tena Bunda Mjini ( Tanzanite)
Januari Makamba amesema kuwa vilabu kadhaa vinahitaji saini yake mwishoni mwa msimu huu ( Habari Leo)
Tetesi zingine magazeti ya kesho
