Makapuku Forum

Martin Fayulu ndiye mgombea wa muungano wa vyama vya upinzani atakayewania kiti cha urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.

Mfanyabiashara huyo maarufu ndiye atakayepambana dhidi ya Emmanuel Ramazani Shadary katika uchaguzi mkuu ujao unaopangiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba.

Rais aliyeko madarakani Joseph Kabila, haruhusiwi kikatiba kugombea tena urais baada ya kukamilisha muhula wa 2
 
”Rais wa Gabon Ali Bongo yuko katika hali mahututi katika hospitali moja nchini Saudi Arabia ” Msemaji wake Ike Ngouoni amesema.

Bongo hajaonekana hadharani kwa majuma kadhaa sasa na kuibua tetesi kuhusiana na hali ya afya ya kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 59.

Kulikuwa na madai kuwa aliugua kiharusi lakini msemaji wake hakulizungumzia wala kuthibitisha “Japo yuko katika hali mahututi rais Bongo anaendelea kupata ahueni "Ngouoni alisema.
 
Bobi Wine: Nyota wa muziki wa pop ambaye pia ni mbunge wa upinzani anayeliwakilisha eneo la Kyadondo East nchini Uganda ameandaa tamasha lake la kwanza la muziki tangu akamatwe na kushtakiwa kwa kosa la uhaini kwa “kumshambulia” rais Yoweri Museveni.
 
Kim Kardashian West na mumewe Kanye West pamoja na mwanamuziki Lady Gaga ni miongoni mwa maelfu ya wenyeji takriban 250,000 wa jimbo la California Marekani ambao wamelazimika kuhama makwao kuepuka moto mkubwa ulioteketeza asili mia kubwa ya jimbo hilo na kuua hadi watu 25.

 
Mamia ya wanawake nchini Iran wameruhusiwa kuhudhuria mechi ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Asia mjini Tehran.

Hatua hii inaonekana kama uwezekano wa kufikisha mwisho zaidi ya miaka 35 ya kutengwa wanawake kutoka mechi muhimu za kandanda.

Walitazama timu ya nyumbani Persepolis ikishindwa na timu ya Japan Kashima Antlers.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…