Kulingana na uchavushaji, nyanya zinagawanyika katika makundi mawaili:
OPV (Open Pollinated Variety) – Hizi ni aina za kawaida
Hybrid – Chotara: Hizi ni nyanya zilizoboreshwa, aina hii zina mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.
Soma hapa mbegu bora mpya za mazao
Hata hivyo katika karne hii ya 21, nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa, zinazo zaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema. Nyanya zinazoonyesha kuwa na sifa ya kuhifadhika bila kuharibika mapema ni kama:
a) Tengeru’97 ambayo ina sifa vifuatazo:
Huzaa sana kutokana na wingi wa matunda na muda mrefu wa kuvuna, ambao hufikia michumo mikubwa kati ya 6-7 kuanzia kuvuna hadi mwisho wa mavuno.
Aina hii ina sifa ya kuwa na ganda gumu, hivyo haziharibiki haraka wakati wa kusafirisha au kuhifadhi (wastani wa siku 20)
Zina sifa ya kuvumilia baadhi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa kunyauka
Tengeru’97 hustahimili mashambulizi ya minyoo fundo (Root knot nematodes)
b) Tanya
Sifa kubwa ya Tanya ni kwamba nayo huzaa sana
Huwa na ganda/ngozi ngumu ambayo inazuia kuoza au kuharibika kwa urahisi wakati wa kusafirisha au wakati wa kuhifadhi kwa muda mrefu.
Tanya nayo ina ladha nzuri inayopendelewa na walaji wengi
Zingatia: Tatizo la Tanya na T97 ni kwamba si kubwa sana kama marglobe 2009. Lakini ukubwa ni karibu unge karibiana, haujapishana sana. Kwa ujumla, ukubwa na wingi wa mazao hutegemea sana matunzo, udongo, hali ya hewa na mazingira kwa ujumla.