MALEZI HAYA NDIO YAMETENGENEZA VIONGOZI TULIONAO SASA! (UTAWALAUMU?)
Kama umezaliwa kabla ya mwaka 1990 utakubaliana na mimi kwa aina hii ya malezi uliyolelewa nayo!
1.Mzazi ndiye Mungu, yaani hata kama umefundishwa kwamba anga ni la bluu, mzazi akikuambia anga lina rangi ya njano inabidi ukubali!
(matokeo yake viongozi hawakotayari kukosolewa)
2. Nyumbani ni kwa ajili ya yeyote ilimradi tu awe ni ndugu, ndugu yeyote anaweza kuja kukaa kwa muda wowote hata kama alifukuzwa kwao hukuna haja ya kuwa na wasiwasi nae maadam ni ndugu yetu!
(matokeo yake, mgeni toka nje akija, No problem! Ni rafiki zetu sana hawa, mpe ardhi)
3.Mdogo kwenye familia ndiye atakaesingiziwa kafanya uharibifu wowote nyumbani, mpaka atakapokuwa na uwezo wa kujitetea!
(Matokeo yake wenye vyeo wakitaka “kula” wanatumia mgongo wa watu Fulani wa chini ambao hawana sauti)