Fisi jike huwa na muonekano wa jinsia mbili, katika uke wake kwa juu au sehemu ambayo mwanamke hukeketwa, ile sehemu kwa fisi huwa na ukubwa mkubwa sana inaweza fika nchi saba, jambo hilo humfanya aonekane na muonekano wa jinsia mbili.
Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula au dume, na kwa bahati mbaya mmoja awe Mdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kama wapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huo dume hubaki likishangaa tuu na kushindwa lianzie wapi.
Usisubutu kumvizia fisi kwa nyuma, namna pekee ya kujirinda hurusha kinyesi chake kwa ghafla na atakuacha ukiwa umechanganyikiwa huku yeye akikimbia.
Uoga kwake huisha akiwa na njaa Kali, kwa mfano hawezi kumuwinda binadamu mkubwa, lakini litokeapo suala la njaa Kali huwa hajali umri wa mtu.
Watoto wake wanapofikisha umri wa miaka miwili mama yao huwatimua, wakajitegemee.
Fisi anapokutana na watoto wa simba huwaua pasina huruma.
Fisi dume halitakagi kusikia habari za watoto, huwa linaamini ni Mali ya jike, hivyo hanaga nao msaada kabisa.
Fisi jike huwa na mwili mkubwa kuliko dume.
Adui yao mkubwa ni mbwa mwitu, kwakuwa huwapora nyama ambazo wao wametafuta kwa tabu sana, pengine kwa kuhatarisha maisha yao.
Fisi wanaogopa sana dume la simba, wanaweza kuwasumbua majike wa simba watatu lakini likija dume huwa linahakikisha mmoja kati yao anachechemea, hivyo wanapomuona simba dume hupiga kelele za kupeana habari kuna hatari.
Fisi ana uwezo mkubwa wa kunusa, hivyo ukifukia kitu hata chini anaweza kukitambua endapo tuu kina harufu ya damu damu.
Viumbe hawa wakijihakikishia akiba ya chakula katika himaya zao, basi hufanya sherehe na sherehe zao huwa na ufanano na sherehe za binadamu, hucheza, hufurahi, hufanya ngono na ugomvi huzuka pia wakati huo watoto wote hufichwa ndani ya nyumba.
Fisi jike huweza kupiga dume mpaka likahama nyumba, na hutumia sana ujanja huu endapo jike linataka kuishi na mchepuko wake ndani.
Fisi huamini pia katika umoja.
****************WANYAMA WABABE KWA FISI *****************
Fisi ni mnyama mnyonge sana na ni mnyama ambaye karibia wanyama wote wawindaji ni wababe kwake, kinachowasaidia ni hali ile ya kutembea makundi makundi yaani kifamilia, ndio huwafanya na wao waonekane kidogo wanajiweza.
***************UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI******************
Kwanza kaa ukijua fisi sio mnyama wa kumchezea, naye ana uwezo wa kukurarua vile vile, usijeanza fikiria zile hadithi za shule ya msingi ukamchukulia pia, sungura mwenyewe akimuona anafungua njia vibaya sana, japokuwa si kiumbe anayevamia moja kwa moja, huuma kwa kuvizia, jihami vya kutosha na uwe na silaha nzuri kama fimbo nzito, mawe yenye ujazo mzito, na usimpe nafasi ya kumuonesha unamuogopa japokuwa kicheko chake chaweza kukutia hofu Mara dufu.
Ukumbuke anapotoa sauti hizo, wenzie wanaposikia hujua kina jambo, hivyo hakikisha haumpi nafasi hiyo, vinginevyo wakiwa zaidi ya wawili andika na wosia kabisa.
*******************************************
Wanyama hawa wapo wa kutosha sehemu kama ngorongoro ni zaidi ya uchafu, mikumi, Serengeti ndio usiseme, hapo hujamalizia na katavi, ni wanyama ambao kibali cha kumuweka kwenye zoo unaweza ukakipata ndani ya muda mfupi sana.