Makapuku Forum

Makapuku Forum

.
Screenshot_20180926-080451.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Moto hauzimiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii hauzimiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii moto na uwakeeeeeeeeeeeeeeeeeeer
tapatalk_1536779357107.gif
 
Tumetoka mbali sana aisee, yaani hapo kunautofauti wa miaka 139
Screenshot_20180926-083324.jpeg
 
Kulingana na ripoti ya World Economic Forum, ifikapo mwaka 2022 nafasi za kazi milioni 72 zitachukuliwa na maroboti Duniani kote, huku nafasi zingine milioni 133 zitaletwa na maroboti hao.
Screenshot_20180926-083437.jpeg
 
Mwaka 2015, watu wengi walikufa kwa ajali za selfie kuliko walioshambuliwa na papa Duniani kote.

Wapenda selfie mpo muangalie na sehemu za kujipiga selfie sio mpaka barabarani au mkiwa mnadrive mtakufwaa

Mwenyewe napenda selfie ila acha niishie hapa

Screenshot_20180926-083548.jpeg
 
Ulimwengu ni sehemu pana iliyojawa na siri nyingi nzito ambazo sisi binadamu tuliokuwa kwenye hiki kidunia chetu kidogo hatutoweza kuja kuzifahamu bali sehemu ndogo sana ya siri hizo tena kwa kupitia darubini kubwa kama Hubble Space Telescope iliyokuwa huko angani ambayo inazidi kutuonesha maajabu ya ulimwengu kwa mfano kama hii picha ambayo imepigwa hivi karibuni na darubini hiyo.

Picha hii unaweza ukasema imechorwa au kitu ambacho kimetoka kwenye filamu ila si kweli bali ni picha halisi iliyopigwa huko nje ya Dunia na kila kitu unachokiona hapo kipo kweli.

Kwenye picha hii kuna mkusanyiko wa galaksi kila moja wapo imebeba nyota ambazo kila moja inazungukwa na sayari, miezi, mawe na uchafu mwingine.

Je? kati ya hizo nyota ni ngapi ambazo zinaweza kuwa na viumbe hai (Aliens)? hatujui na hatutokuja kujua kamwe kwa sababu kama tukisema tuanze safari ya kwenda huko sasa, hiyo ndege itatumia miaka 100,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000,000 mpaka kufika huko
Screenshot_20180926-083808.jpeg
 
Chombo cha NASA kinachofahamika kama Parker Solar Probe, ambacho kwa sasa kinaelekea kwenye Jua kimeanza kutuma picha za kwanza.

Parker Solar Probe kimetuma picha ya muonekano wa galaksi yetu ya Milky Way wakati kikiwa kinaelekea kwenye Jua katika safari ambayo itakichukua miaka saba mpaka kufika kwenye Jua, na kukumbana na joto ambalo linafikia nyuzi milioni moja kwenye uso wa Jua ikiwa ni sehemu ya kutaka kufahamu jinsi Jua letu linavyofanya kazi.
Screenshot_20180926-083946.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Hii picha ilipigwa na chombo kinachofahamika kama Rover-1A kutoka shirika la safari za anga za majuu Japani (JAXA) wakati chombo hicho kikitua kwenye jiwe kubwa linalofahamika kama Ryugu lililokuwa umbali wa maili milioni 180 kutoka Duniani au sawa na mara mbili ya umbali kutoka Duniani mpaka kwenye Jua.

Kwa sasa Japani ndiyo nchi pekee ambayo imeweza kutuisha chombo kwenye Jiwe kubwa ambalo linalosongea huko angani.
Screenshot_20180926-084100.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Obe

Similar Discussions

Back
Top Bottom