Makapuku Forum

Makapuku Forum

_103256046_914229848-594x594.jpg

Afisa mpya mtendaji wa klabu ya Aston Villa Christian Purslow anatarajiwa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati Jack Grealish kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.. (Telegraph)
 
Beki wa Portugal Diogo Dalot, 19, ameichezea mara ya kwanza Man United tangu uhamisho wake wa dau la £19m akiichezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 kwa dakika 79 (Manchester United website)
 
John Terry na Jack Grealish walisaidia kumshawishi mshambuliaji wa Uingereza na Chelsea Tammy Abraham, 20, kujiunga na Aston Villa kwa mkopo. (Express and Star)
 
Wakati huohuo kiungo wa kati wa Armenian Henrikh Mkhitaryan, 29, huenda asiichezee Arsenal wakati watakapocheza dhidi ya Qarabag FK katika kombe la Yuropa kwa sababu ya mgogoro wa kisiasa kati ya Armenia na Azerbaijan. (Mirror)
 
Jurgen Klopp hajakubali kwamba winga wa Liverpool Mohamed Salah, 26, bado anataka kuichezea timu yake ya taifa na kwamba anatumai kwamba suluhu mwafaka itaangaziwa kuhusu mgogoro wake na shirikisho la soka nchini Misri.(Mail)
 
Maurizio Sarri anasema kuwa kiungo wakati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 22, anahitaji kuimarika kiufundi ili kuweza kushiriki katika kikosi cha kwanza cha timu. (Metro)
 
_103247721_tv048896529.jpg

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atakuwa mmojawapo wa wakufunzi bora zaidi duniani hata iwapo hatposhinda ligi ya Uingereza na klabu hiyo.

United imepoteza mewchi mbili kati ya tatu iliocheza , ikiwa ni mwanzpo mbauya tangu mwaka 1992-93.

Akitetea rekodi yake , mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 55 alisema kuwa ndio meneja wa pekee kushinda mataji ya ligi akiwa Itali, Uhispania na Uingereza.

Pia amesema kuwa ****;liza katika nafasi ya pili katika ligi hiyo ni mojwapo ya ufanisi mkubwa. Alipoulizwa iwapo atakuwa miongoni mwa wakufunzi bora iwapo hatoshinda taji la ligi ya Uingereza na man United , alijibu ndio.

Mourinho amejitetea kuhusu kazi yake siku chache tu baada ya timu yake kulazwa 3-0 na Tottenhama katika uwanja wa Old Trafford.-ikiwa ndio matokeo mabaya zaidi ya nyumbani katika ukufunzi wa Mourinho.
 
Alitawataka waandishi habari kumuheshimu , na kuwakumbusha kwamba mataji mataytu ya ligi ya Uingereza alioshinda awali na Chelsea ni zaidi ya wakufunzi wote walioshinda wakiwa Uingereza.

kabla ya mechi yake dhidi ya Burnley siku ya Jumapili, raia huyo wa Ureno aliongeza: Nilifanikiwa pakubwa msimu uliopita na hilo ndio swala ambalo hamtaki kulkubali.

Misimu miwili iliopita tulikuwa na msimu mzuri ka sababu tulishinda taji la Yuropa. Tulishinda kwa sababu lilikuwa katika viwango vyetu. man United ndio timu ya mwisho Uingereza kushinda taji la Yuropa.

Mimi ndio meneja wa pekee kushinda mataji manane Italy, Uhispania na Uingereza-sio mataji madogo-na kuibuka wa pili msimu uliopita ni miongoni mwa ufanisi mkubwa niliopata.
 
Wakati Mourinho alipoambiwa kwamba mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alikabiliwa na maswali kama hayo msimu uliopita, Mourinho alijibu: kwa sababu hakushinda chochote katika soka ya kimataifa.

"Hilo ni tataizo lake , ninawaambia kile ninachofikiria, na vile ninavyohisi. Na ninajibu swali.
 
Marekani yasitisha kutoa misaada kwa Palestina

Marekani imesema kuwa imesitisha ufadhili kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, hatua inayotishia kuzidisha mzozo kati ya Palestina na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Msemaji wa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amelaani uamuzi huo wa Marekani ambao ameutaja kama hatua ya kuwadunisha Wapalestina na inayoendana kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Aidha, kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Heather Nauert amesema kuwa operesheni na muundo wa shirika hilo la UNRWA una mapungufu makubwa na baada ya tathmini ya kina, Marekani imeamua kusitisha ufadhili.

Marekani huchangia karibu asilimia 30 ya bajeti ya shirika hilo ambalo husaidia kutoa huduma ya afya, elimu na huduma nyingine kwa wapalestina takriban milioni 5 katika ukanda wa Gaza, ukingo wa Magharibi mwa Jordan, Syria na Lebanon.

Wengi wa wakimbizi hao ni watu waliokimbia vita vya mwaka 1948 ambavyo vilipelekea kuundwa kwa taifa la Israel ambalo limekuwa katika mgogoro na nchi za mashariki ya kati.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump na maafisa wa utawala wake wamesema kuwa wanataka kuboresha maisha ya Wapalestina na pia kuyafufua mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina.
 
Makontena ya Makonda Yakosa Wateja Tena

Muungwana Blog 2 Saturday, September 01, 2018



MNADA wa makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, umefanyika leo Jumamosi, Septemba 1, 2018 katika Bandari ya Dar, lakini imeshindikana kupatikana mnunuzi, hivyo mnada huo utaendelea Jumamosi ijayo.

Mkurugenzi wa kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Scolastika Kevala, amesema hawajapata mnunuzi wa kontena hata moja lakini wamefanikiwa kuuza bidhaa 10 tu zilizokuwemo kwenye makontena hayo.

Sehemu kubwa ya bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati na vitu vingine.

“Mpaka sasa tayari tumefanya mnada wa makontena yote 20 lakini hayajapata mteja ingawa tumefanikiwa kuuza bidhaa 10 zilizokuwemo kwenye makontena hayo. Hivyo mnada wa makontena utaendelea tena Jumamosi ijayo,” amesema Kevela.

Itakumbukwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango aliagiza makontena hayo kupigwa mnada licha ya RC Makonda kutoa vitisho kuwa atakayenunua vitu vilivyomo kwenye makontena hayo atapata laana.

Aidha, mnada wa makontena hayo unakuja ikiwa ni baada ya Makonda kushindwa kuyalipia kodi kiasi cha Tsh. Bilioni 1.2.
 
Guardiola amtolea uvivu, Mourinho

Muungwana Blog 2 Saturday, September 01, 2018



Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa kamwe hatamhukumu, Jose Mourinho kwa kauli yake aliyo waambia waandishi wa habari kumpatia heshima yake kwa kuwa ametwaa mataji matatu ya ligi kuu England kuliko kocha mwingine yoyote waliyopo sasa.

Kauli hiyo ya Mourinho imejiri baada ya kupoteza mfululizo kwenye michezo yake ya mwanzo wa ligi mbele ya Brighton na Tottenham. Wakati meneja wa Manchester City, Guardiola alipoulizwa juu ya kauli hiyo ya Mourinho amesema kuwa hawezi kuukumu hilo.

Kocha Pep Guardiola akiwa amekumbatiana na Jose Mourinho baada ya mchezo wao

”Siwezi kuukumu hilo isipokuwa wapo makocha wengi waliyo bora na hawaja fanikiwa kushinda mataji ndiyo maana kwa upande wanguna naweza kusema inatokea kushinda kwakuwa unakitu cha ziada kinachokufanya ufanikiwe hilo, hata hao mameneja wazuri wanashindwa kushinda ubingwa kutokana na hicho kitu cha ziada kukosa kama vile klabu nzuri yenye wachezaji waliyo na viwango vya hali ya juu,” amesema Guardiola.

Pep Guardiola ameongeza “Nimelisema hilo mara kadhaa kwa mfano hata mimi mwenyewe nimeshinda mataji kwa sababu nilikuwa kwenye klabu kubwa zenye wachezaji bora na kama hilo lisingekuwa nisingeshinda hata ubingwa.” Hata hivyo Mhispania huyo hakusita kumpa heshima yake Mourinho kwakusema kuwa hakuwahi kuwa na shaka na ubora wake hivyo hata leo itaendelea kuwa hivyo lakini siyo kwa sababu ya mataji tu.
 
Mabao ya Kagere yafutwa Simba

Muungwana Blog 2 Saturday, September 01, 2018




LICHA ya straika wa Simba, Meddie Kagere kufunga mabao matatu mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems amesema anaona haitoshi hivyo anahitaji zaidi ya hayo.

Kagere kwa sasa ndiye kinara wa mabao Simba na Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mabao matatu kwenye michezo miwili aliyocheza ambayo ni dhidi ya Prisons alitupia bao moja na Mbeya City mabao mawili.

Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumamosi kuwa, straika wake huyo anatakiwa kuongeza kasi zaidi ili afunge mabao mengi yatakayosaidia kuibeba timu hiyo na kutetea ubingwa wao wa ligi kuu.

“Siyo mbaya kwa namna ambavyo amekuwa akifanya japo kwangu naona bado haitoshi anatakiwa kufunga zaidi na zaidi kadiri ya timu itakavyoshuka dimbani lakini kutengeneza nafasi kwa wenzake kwa ajili ya kupata mabao.

“Yeye ni mmoja wa washambuliaji wazuri tulionao hapa na lazima aonyeshe makali yake kwa kufunga katika michezo yetu,” alisema Mbelgiji huyo.
 
Gari la Waziri wa Afya Nusura Liue Mwendesha Baiskeli

Muungwana Blog 2 Saturday, September 01, 2018



Mkazi wa Kata ya Ngogwa, Kahama mkoani Shinyanga, Marco Charles (48), amenusurika kifo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili STL 2777 lililokuwa limembeba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy alikuwa akitokea mkoani Kagera kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 27 majira ya saa 10.30 jioni, eneo la Ngogwa barabara ya Masumbwe kuelekea Kahama.

Kamanda Haule alisema gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Jumanne Ally (45), dereva wa Waziri Ummy Mwalimu, lilikuwa likitokea Ngara mkoani Kagera kwenda Dodoma ndipo lilimgonga mwendesha baiskeli, Marco Charles (48) na kumsababishia majeraha kichwani, mkono wa kulia na shingoni.

Haule aliongeza kuwa, kutokana na ajali hiyo, majeruhi huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama na anaendelea na matibabu.

Wakati huohuo, Kamanada Haule alisema tarehe 26 majira ya saa 9.53 usiku mtaa wa Nyasubi katika baa ya Chillar Kahama mjini, Emmanuel Philimon (39), mlinzi wa baa hiyo, alijeruhiwa kwa kupigwa na risasi katika mapaja yote mawili na George Nyamhanga (41), ambaye ni mhasibu wa baa hiyo.

Ilielezwa kuwa, alifanya hivyo wakati akisaidia kuwazuia watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kumjeruhi mlinzi mwingine wa baa hiyo, Baharia Athumani (25), mkazi wa Nyasubi aliyepigwa na chupa.

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo ni uzembe wa mtumiaji wa bastola hiyo yenye namba za usajili 785819 CAR Na. 00104206 aina ya Browning, kutochukua tahadhari za kutosha wakati akifyatua risasi hewani ili kuwatuliza watuhumiwa watatu wasitoroke.

Watuhumiwa hao walikuwa wamekamatwa kwa kumpiga chupa mlinzi huyo.

Kamanda alisema mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo kwa uchunguzi zaidi na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri.
 
Yanga FC yaanza mikwara

Muungwana Blog 2 Saturday, September 01, 2018



MWINYI Zahera yuko DR Congo akiifundisha timu ya Taifa ya nchi hiyo lakini amewaambia Simba wajiandae kwavile Yanga sasa ipo tayari kwa mapambano.

Zahera ambaye ni kocha msaidizi wa DR Congo hatokuwa kwenye kikosi cha Yanga kitakachocheza mechi ya kirafiki dhidi ya Singida United Septemba 5, mwaka huu mkoani Kigoma kutokana na kuwa na majukumu mengine.

Ameliambia Championi Jumamosi kuwa, haoni tabu tena kwenye kikosi chake kama ilivyokuwa huko nyuma ambapo wachezaji wengi walikuwa na migomo ya hapa na pale, lakini sasa suala hilo limekwisha kilichobaki ni kazikazi hivyo timui pinzani zijiandae ikiwemo Simba.

“Nina kikosi kizuri sana hasa ukiangalia umri wa wachezaji wangu bado ni bora zaidi ya wengine jambo linalonipa moyo kuwa tutafanya vizuri sana kwenye ligi maana kikosi changu ni kipana na kinatosha kabisa kugawika hata kwa uwiano wa michezo sawa ya ligi,”alisema Kocha huyo ambaye anaishi karibu na ufukwe wa Bahari ya Hindi upande wa Kawe.

“Hadi sasa nina safu bora ya ushambuliaji tofauti na wengi kuendelea kumtazama Makambo (Heritier) pekee wakati nina watu wazuri kama Matheo (Anthony), Mhilu (Yusuf), Nkomola (Yohana) na wengine wengi kama kina Kaseke na Mrisho Ngassa na hawa wote wanaumri mzuri unaoweza kurekebisha na kuja kufanya maajabu nje ya matarajio ya wengi.

“Kuna watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa Simba tu ndio ina mtaji wa mastraika huku wakiibeza Yanga jambo ambalo si kweli kama tuna kikosi kibovu kiasi hicho na ukitaka kufahamu kuwa Yanga ina vikosi zaidi ya viwili basi ni nafasi ya kila mmoja kusubiria mbio za ligi zizidi kusonga na baadaye wataona ninachokimaanisha,” alisema Zahera.
 
Kondoa imewafikisha mahakamani askari wanyamapori watatu wa pori la akiba la Mkungunero kwa kosa la kuomba rushwa ya Shilingi milioni nne.

Washtakiwa hao Steer Waliya, David Kayila na Nginanu Olepesa, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kondoa wakituhumiwa kukamata ng'ombe 88 walioingia kwenye hifadhi na kupokea rushwa kutoka kwa wamiliki wa mifugo hiyo ili waiachie.

Wilayani Mpwapwa, Takukuru imemfikisha katika mahakama ya wilaya hiyo Lazaro Masimami, ambaye ni Ofisa Ardhi Msaidizi wa halmashauri ya wilaya kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh. 300,000 kwa mwananchi mmoja, ili amsaidie kupata hati ya kiwanja chake.

Wakati huo huo, Takukuru hivi karibuni imeshinda kesi ilizokuwa inaendesha wilayani Kondoa na Mpwapwa kwa mshtakiwa Saidi Abdalah, kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya Sh. 500,000 baada ya kutiwa hatiani kwenye shtaka la ubadhirifu na ufujaji na pia alitakiwa kurejesha Sh. 2,859,050 alizofuja wakati akiwa katibu wa kamati ya maji wa Kijiji cha Mwaikisabe, wilayani humo.

Aidha, Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa imewatia hatiani na kuwahukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini, walimu wawili wa Shule ya Msingi Idilo, Henry Kindole na Peter Joctan, waliokuwa wanakabiliwa na shtaka la ufujaji na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa shule hiyo.
 
Back
Top Bottom