Makapuku Forum

Muziki: Tutajuana Tu

...usiwe na wasiwasi na kichwa cha habari, utamu uko kichwani na ndo maana hata kumuua nyoka unapiga kichwa na wengine ukimlamba kichwa ndo unamkasirisha vita yake haitanipa hata nafasi ya kukusalimia wewe Kapuku unayelifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo. Asante sana aunt yangu Shunie kwa kuweka magazeti na Je wajua, ukweli ni kuwa, muungwana ni jadi yake kushukuru (acknowledge) mazuri yanayofanywa na mmoja au wengi. Nami nafanya hivyo kila muda nikipata nafasi.

Ninajua kabisa, ungeweza kuweka mabandiko yako sehemu nyingine na ama kuanzisha uzi kuzihusu, lakini umetupa heshima Makapuku kuzisoma kwanza na ndiyo maana hapa panakuwa ni pazuri kuwepo kwa sababu wadau wa ukweli wanakuwepo hapa. Utofauti wa MF na majukwaa mengine ni kuwa hapa ni kama bahari, maarifa, burudani na sogozi zinapatikana, ni muda wako tu.

Muziki sasa, nisikuchoshe ila nikukumbushe tu kuwa kesho ni Jumatano, kama huna kalenda sema asante..

 
Mkuu kwema
 
Wouuuuzeeeer wouzeeeerr
binamu santeee
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…