TUOMBE:BWANA YESU ASANTE kutuamsha salama leo Jumatatu 16 Julai 2018.Wako wengi walitamani kuiona leo hawajaweza tunakurudishia Sifa ,Shukurani,Heshima na Utukufu kwako Mungu na Baba yetu uliye juu.
Tunaomba Toba Baba Uturehemu.
Tunaomba huruma yako isiyopungua siku hadi siku iwe nasi.
Asante kwa Upendo wako na kutuheshimisha kusiko mwisho.
Asante kwa sababu ya familia zetu watoto wetu wa kike na kiume wamekua baraka kwetu,endelea kuwakumbatia na kuwapa haja ya mioyo yao...Baba waepushe na hatari zote za Mwili na Roho wapiganie katika kila hatua za maisha masomo,kazi,mahusiano waponye majeraha yote na mioyo iliyovunjika waaambie kila siku kwako lipo tumaini na kwako Kuna USHINDI..Hakuna kuchelewa wala kuwahi kila jambo lipo kwa majira ambayo kila mmoja anayo majira na wakati wake.
Asante Baba kwa Baraka ya kazi za mikono yetu mashamba kazi ujasiriamali endelea kutubariki.
Ponya wagonjwa watie nguvu wajane wagane,yatima wafariji wafiwa wape tumaini
Tunaomba anza nasi na maliza nasi wiki nzima inayoanza leo.
Roho Mtakatifu Tufundishe kuishi maisha Matakatifu.
Tunaomba na kuamini katika jina la Yesu Kristo lipitalo majina yote Amen
WIKI NA JUMATATU NJEMA DAMU TAKATIFU YA YESU KRISTO ITUFUNIKE