Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Picha Yako, Thamani Yako

....kama utakuwa umegundua kitu leo, muziki umekuja mwanzo wa Tafasiri Unavyoweza, maana yake ni kuwa ninakusalimia kwanza na kukufahamisha kuwa T.U haitokuwepo leo kutokana na sababu zilizo ndani ya uwezo wangu. Ni jambo zuri kukuona hapa kila wakati na ni wewe pekee ndo unalifanya jukwaa hili kuwa jukwaa la kipekee kabisa hapa JF. Yapo majukwaa mengi mazuri, lakini kwangu mimi sababu ya uwepo wako hapa Makapuku Forum ni jukwaa bora zaidi. Unaweza kutafasiri unavyoweza.

Nilikuwa na wikend ngumu kidogo, nilikueleza kuwa nilifunga na nikashindia uji wa malimau na ukwaju maana si kwa kikohozi na mafua kutokana na vumbi linaloletwa na mvua zinazonyesha sasa hivi. Anyway, siwezi kulalamika maana malalamiko yangu hayawezi kunisaidia kama sijaamua kuchukua hatua mwenyewe. Nisikuchoshe na kabobo wakati kipengele hiki ni kwa ajili ya burudani.

Muziki sasa, asante kwako wewe unayenisoma sasa hivi na hongera kwa wote ambao mmelichangamsha jukwaa kwa sogozi zinazovutia, ila mzeewakungoa kampeni yako si ya karne hii, nakutakia mafanikio na umebadili picha naona khali si mbaya, na uliniuliza kama nina utani na wewe, la, sina utani yale mambo ya mwarabu koko unamjua aliyeyaanzisha.

 
Back
Top Bottom