Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Tunaangukia Wapi?

Maendeleo ni dhana pana sana kuiongelea na katika kuitafasiri bado inachanganya lakini pamoja na kuchanganya kwake huku bado wengi tunakubaliana na ukweli kuwa maendeleo ni kuwepo kwa mabadiliko (social change) yanayoruhusu watu kufikia malengo yao katika maisha (human potential). Maendeleo ni ile hali ambayo angalau unakuwa na uwezo wa kutimiza na kupata mahitaji yako kikamilifu. Kiurahisi rahisi tu, kama nchi ina rasilimali za asili, ardhi, madini, mafuta n.k, na kama haina hivi vitu basi wananchi kuwa na elimu ni njia ya kuwa na mendeleo. Sisi tuna cha kwanza, maliasili na cha pili ni mtihani, elimu tunaijengea matabaka na baadhi wanaona ni sawa. Serikali inawajibika kutoa elimu bora kwa watu wake. Tafasiri Unavyoweza

Inashangaza sana kwa kiongozi kuanza kusema kuwa serikali itatoa elimu kibaguzi, kwamba kama mzazi wako ana leseni ya biashara basi sahau mkopo elimu ya juu, na kwamba kama umesoma shule binafsi napo sahau mkopo. Ni jukumu la serikali kutoa elimu bora kwa wananchi wake. Tunajua kabisa tumeshindwa kwenye kuzifanya maliasili tulizonazo zilete maendeleo, na hili wa kulaumiwa ni serikali. Awamu iliyopita ililenga kutoa elimu kwa wengi na kuimarisha vyuo vya kati, hii ilikuwa ni njia nzuri ya kuleta maendeleo maana elimu haidanganyi. Kwenye uchumi, faida za elimu zinaitwa 'positive externalities' maana yake mwenye elimu anamfaidisha yeyote anayemzunguka. Mfano, mwalimu, daktari nk.

Sisi tunaangukia wapi kama rasilimali tulizonazo tumekuwa tukizigawa kwa zawadi za kijingajinga kabisa, zawadi zinazoisha kesho (perishables) na sasa elimu tunaifanya iwe ya wachache. serikali ni jukumu lake kutoa elimu kwa wananchi wake, japo inawezekana ikawa ni ndoto, yapo mataifa hayana rasilimali za asili kama sisi na yakajikita kwenye kuwaelimisha vijana wake na leo yanashindana na mataifa ambayo yanatumia mali za asili yalizojaliwa kuwaletea maendeleo wananchi wake. tafakari na jiulize sisi tunaangukia wapi ikiwa bado hatujaanguka kabisa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…