Binamu asanteTafasiri Unavyoweza! Akili Ni Kuhoji Sio Kunyamaa
Hakuna ubishi kuwa zama zinabadilika sana, hata walio ndani ya boksi wanapata nafasi ya kunyanyua vichwa vyao kuona ndani ya boksi kuna nini maana kila siku wanaambiwa kutazama nje ya boksi. Ukweli ni kuwa huwezi kuona kilicho nje ya boksi kama kilichomo ndani ya boksi ulimokaa hukijui. watu sasa wanahoji maana wanauelewa wa mengi, huwezi kukaa unawadanganya maana huwezi kuwadanganya watu wote muda wote. Tafasiri Unavyoweza.
Kuna viongozi kila wakifungua vinywa vyao baada ya kula mapochopocho kwenye majumba tunayowalipia kukaa hawaishi kusema yanayowafurahisha na kulinda maslahi yao pekee na si vinginevyo. Wanaenda mbali zaidi na kutaka kutufundisha namna ya kufikiri. Hawataki tusome na tuhoji, wanatamani kuongoza malaika ili watufanye sisis kondoo, ttusioweza kuinua vichwa na kuangalia mbele kuna nini ikiwa wao wametangulia.
Wanatumia pesa kwa utashi wao bila kuleta mrejesho na mbaya zaidi wanatumia pesa hizi kwa manufaa yao binafsi na kutuletea viswahili vingi tukitaka kujua matumizi mapato yaliyofanya. Tukatae ukondoo, tuwe na shauku ya kuhoji maana kuhoji ndo akili vinginevyo ukimya wako ndo hasara yako na kiama ya kizazi chako maana kizazi cha kiongozi kinafundishwa kuendeleea kukuibia na kukuongoza.
[emoji3] [emoji3] [emoji3]Hatimae tumerudi hewani
Woooozeee huko apiii sasa bday boy nimekutana nae mitaa ya kati hukoNmekuja kumtakia kheri ya kuzaliwa baba wawili
Mungu amtimizie haja ya moyo wake
Ampe miaka mingi ya kuishi duniani
Obe ukipita hapa mchagulie wimbo mzuri aburudike pamoja na makapuku wote
HBD Shululu
Ulipotelea wapi jamani[emoji16][emoji16][emoji16]
WoyoooooooooooooHatimae tumerudi hewani
Mhh nilitekwa acha tu,ila nilikumisini jamenUlipotelea wapi jamani
Jamani tulikumiss pia najua ulitekwa kwa raha karibu tena mamyMhh nilitekwa acha tu,ila nilikumisini jamen
Naunga mkono hoja binamuTafasiri Unavyoweza: Maandamano Yamelipa
Hakuna ubishi kuwa leo maandamano yamefanyika, ndiyo yamefanyika tena kwa kiwango kikubwa sana. Maandamano haya unaweza kuyatafasiri unavyoweza nami nitakueleza kuwa wakati wewe ulikaa ndani leo polisi wengi kwa karibu wiki nzima hii walikuwa wakiandamana (wenyewe wakiita mazoezi) kumuunga mkono dada jasiri (hata kama hukubaliani na baadhi ya mbinu zake za kuwasilisha ujumbe) Mange Kimambi. Ukiwaacha polisi walioandamana kwa wingi sana, raia wengi walikuwa na ufahamu wa tukio la maandamano ya leo na kwa kuunga mkono maandamano haya waliandamana kifikra. Tafasiri unavyoweza.
Ujumbe umetumwa na umefika kikamilifu, ni bahati mbaya sana kuona rais na serikali inayojinasibu kufanya mambo mazuri inakuwa katika nafasi ya kujihami zaidi kuliko kujitokeza nje na kusikiliza yale ambayo yanasemwa kuwa haifanyi. Haki ya kujieleza kama ilivyo haki ya kuandamano na mikutano ni kitu kilichokubaliwa ndani ya katiba, si hisani ya rais, au chama kilichoko madarakani. Ni ushamba mkubwa kudhani kuwa mtu mmoja au kikundi cha kisiasa kinaweza kuamua tofauti na katiba. Ni suala la muda tu, bubu atasema kwa kupaza sauti na hapo ndo walioshika madaraka watapazwa kwa kasi ya kobe, waugulie maumivu kwa kila hatua. Sio utabiri huu ninaoandika, naandika utafasiri unavyoweza.
Asanteni sana jeshi la polisi kwa kuandamano na kumfanya Mange na hoja zake ziwe na mashiko, bahati mbaya sana wakati mnaandamana hakukuwa na chombo kingine cha kuwazuia kuandamana
Asante binamu yangu mm jamani pole na ww...marahaba aunt, pole na maandamano