Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 44,009
- 150,544
Shemuu mwenyeweHbr ya asubuhi wapendwa[emoji113] [emoji113] [emoji113] [emoji113]
Shemuu mwenyeweHbr ya asubuhi wapendwa[emoji113] [emoji113] [emoji113] [emoji113]
Nambie shemela hamjambo ww na familia ykoShemuu mwenyewe
Niko hapa ukimalizwa kutekwa utaniambiaMama d nakumisiiiiii
Mke mwee habari ya weweNambie shemela hamjambo ww na familia yko
Binamu nyimbo nzuri hiii enzi hizo nipo katotoMuziki: Tufurahi Pamoja Sikitika Peke Yako
Kuna mengi yanaendelea na mengine yanavutia machoni na masikioni ila mengine kama ilivyo kwa kila chenye sura basi hakikosi kisogo, mengine yanaumiza na kukarahisha lakini maisha ni lazima yaendelee. Haijalishi umekuwa na wiki ya namna gani, leo ni mwanzo wa mapumziko, weekend nami kama kwaida, nakusalimi na kukutakia mapumziko mazuri maana bila wewe kuwepo hapa, Jukwaa hili linabaki kuwa si sehemu nzuri kuwepo.
Muziki sasa, nimekuona mdau shululu kwa mbali, najua ukikamilisha unachofanya utakuja kulisongesha gurudumu letu hapa.
Nzuri kpenz mekumissMke mwee habari ya wewe
Mkuu obe,Tafasiri Unavyoweza: Usinilaumu, Onesha Umefikaje Ulipo
Hakuna ubishi kuwa wapo baadhi wamejifanya na kujizoesha kuwa wavivu wa kila kitu, hawapendi kujishughulisha na chochote. Wanategemea mbeleko za kila namna (free riders) na hata mambo ambayo yako ndani ya uwezo wao kabisa kufanya hawafanyi. Hawa ni wachache sana katika wengi ambao kila kukicha wanajitahdi kupambana kuondokana na umaskini kwa kufanya kazi, kutia bidii katika yale halali wanayofanya. Hawa ndo msingi wa kipengele hiki cha leo, wanahitaji maelekezo na mbinu za kufanikiwa ulipo na wala huna haja ya kukaa unawalaumu kwa kushindwa kwao kufanikiwa.
Mafanikio yako leo usiyafanye kama mafanikio ya wazee wetu wa zamani ambao walipofariki basi na mafanikio yalipotea. Mafanikio endelevu hurithishwa na si uishie kutoa msaada tu wakati unatakiwa kutoa ndoano na kumfundisha mmoja namna ya kuvua samaki.
tumekuwa na tatizo la kuficha siri za mafanikio yetu tuliyonayo, nia na uthubutu wa mmoja hauwezi kufanikiwa kama hakuna waliotangulia kufika watamshika mkono na kumwelekeza namna sahihi ya kufikia walipo na kwenda mbele zaidi. Tafasiri unavyoweza inamaliza kwa kusema usiishie tu kulaumu mwingine wakati hujaweza kuonesha namna unavyoweza kuondoa lawama kwa unayemlaumu.
Mmmh ubize huo mbona siku zote haukuwepo?Watu wako busy
Aksanteh mkuu, somo makini sana.Tafasiri Unavyoweza: Ujinga Ni Kutosema
Najua kabisa naandika ikiwa ni mwanzo wa mapumziko ya mwisho wa wiki. Kawaida sana huwa sipendi kuandika mambo magumu na ya kufikirisha sana maana hata nami ninahitaji, kama ulivyo wewe, mapumziko ya kurudisha kilichopotea na nilichokosa kwa siku tano za kazi. Ninaandika magumu leo kwa sababu tu ya kuwepo kwa nia ya kufumba jamii mdomo, isiongee, isihoji na wala isiwe na maoni tofauti na wenye kukasimiwa madaraka. Taifa sio viongozi na kwa kuwa taifa letu tumeamua kuwaamini wachache kuongoza basi haimaanishi kuwa wao wanao uwezo wa kufikiria na kutuamulia wanachotaka wao binafsi au taasisi wanazoziongoza. Hii ni kwa sababu si wote wenye maslahi timamu kwa taifa, wengine ni kutaka kujineemesha wenyewe na tunaliona sana hili kwa sasa.
Bunge halifanyi kazi yake, linakutana kutegemea huruma za dola ambayo nayo inatoa masharti mengi tu ili bunge na mahakama ziendelee kuilamba miguu dola. Upo ushahidi wa maneno na vitendo vya wakuu wa taasisi hizi mbili wakijipendekeza vilivyo kwa taasisi dola ambayo kiongozi wake anatamani kuwa kila kitu, awe IGP, awe rais wa Znz awe kamishna wa kodi awe mkuu wa bandari, awe mpiga ngoma, awe 'stedishoo' na lolote unaloweza kutaja.
Bunge butu, bunge kibogoyo, bunge linalowafanya wabunge waingie na 'power bank' kwa sababu hakuna kinachojadiliwa cha maana na hivyo bora mbunge aendelee kucheza game au kutizama mitandao wakati wa mijadala ya bunge. Bunge linaloamua kupeleka taarifa yake ya uchunguzi kwa serikali bila kwanza kuijadili. Ukiwa unadhani ninaandika hisia basi jipe muda wa kufuatilia majukumu ya bunge na uangalie kinachofanyika sasa, tafasiri unavyoweza.
Bunge linaloongozwa na baadhi ya viongozi wanaowakilisha wapiga kura wajinga, ndiyo wapiga kura wajinga ambao hawajui thamani ya kura waliyoipiga, wanapiga kwa mazoea na hivyo kuendelea kuaminin wanachoambiwa na nambunge hata kama ni cha uongo ilmradi tu walikula wali nyama na kilo ya chumvi wakati wa kampeni za uchaguzi.
Ukikaa kimya bila kuongelea udhalimu na unyang'anyi unaofanywa na bunge hili la sasa usijedhani uko salama na ukaendelea kukenua meno kwa viongozi wasiotaka kusikia maoni mengine na hasa wasiyoyapenda. Hakuna mnafiki anayekufa mara mbili. Uwe na mapumziko mema.
Tukutane wiki lijalo.
Habar si mbaya, shemu uzima upoHbr ya asubuhi wapendwa[emoji113] [emoji113] [emoji113] [emoji113]
Sie tu wazima kwa niaba ya wote ambao hatuko tagged.Na makapuku wote nawasalimia sana
[emoji23][emoji23][emoji23]Niko hapa ukimalizwa kutekwa utaniambia
Shedede mamboMmmh ubize huo mbona siku zote haukuwepo?