Makapuku Forum

Makapuku Forum

Napumzika huwa naingia kusoma hadithi tu
...kama uliambiana na Sakayo , jana aliiomba na nikaiweka, nyimbo ya mwaka 74 wewe mtoto wa 89 unaitaka ya nini?
Kumbe sakayo aliiomba tatizo sifukui makaburi binamu halaf me ni muhenga sio mtoto wa 89
 
Kumbe sakayo aliiomba tatizo sifukui makaburi binamu halaf me ni muhenga sio mtoto wa 89

...ha hahahah, ninyi watoto wa siku hizi mmeisoma TOT na Muungano cultural troupe mmeisoma mtandaoni, Sumaku mmemjulia Mizengwe wakati Mandela ya Jangala ndo ilikuwa kila kitu
 
...ha hahahah, ninyi watoto wa siku hizi mmeisoma TOT na Muungano cultural troupe mmeisoma mtandaoni, Sumaku mmemjulia Mizengwe wakati Mandela ya Jangala ndo ilikuwa kila kitu
Hapana binamu Tot na Muungano nakumbuka nipo mtoto nimeenda sana kuangalia michezo yao ya kibisa na mijoka yao woiiii nimetaja hiyo midude huku natetemeka naiogopa mm

Binamu kumbe sumaku alikuwa Mandela ya jangala me najua kaibukia mizengwe tu
 
...kumbe unayajua na majoka yale basi nimeacha, lol! Unastahili kuingia kwenye kundi la mafundi, ndo maana anko wangu hageuki kila akijidai kujipapatua anarudi, mwanzoni nilidhani ni dawa kumbe roho ndo mwamuzi.

Anko wangu Lyon Lee burudika na hiki kibao

Tafasiri Unavyoweza: Hasira Itusaidie, Isiumize

....nilikuwa nikishangazwa sana na namna kamanda mmoja mstaafu wa jeshi la polisi ambaye kila akiongea alikuwa akionesha hasira hata kama taarifa anayotoa ilikuwa ni ya kuelezea jambo la kawaida sana kwenye nchi za kidemokrasia, maandamano. Hasira ni tabia ambayo kila binadamu anayo, wala usijisikie vibaya kuwa nayo, ila ujisikie vibaya pale hasira uliyonayo inakuwa na lengo la kuumiza, kuua na uharibifu kwa mwingine au vitu (hostile aggression). Hii ni hasira mbaya, haikusaidii wewe wala huyo/hicho unachonuia kukionesha upungufu wako. Tafasiri Unavyoweza

Hasira inaweza kukusaidia, ndiyo pale unapoifanya na kuitumia kufikia lengo jema kabisa kama kutia bidii darasani (instrumental aggresion). Hasira ya kufanya kazi kwa bidii, hasira ya kutimiza ahadi ulizoahidi na hasira ya kuwa mwananchi anayewajibika kwa jamii yake. Muangalie mwanajeshi kwa mfano akiwa vitani kwa lengo la kulinda mipaka ya nchi yake, hii ndo hasira unayopaswa kuwa nayo, mwangalie mwalimu anayeadhibu kwa kufundisha uelewe, jiangalie nawe unapojitahidi kufanya kazi kwa bidii kujipatia maisha yenye furaha.

Usiitumie hasira katili/ovu (hostile) popote pale iwe ni moja kwa moja au kificho (indirect aggression- ambapo unakaa kusambaza uongo na fitna kwa lengo la kuumiza au kuharibu taswira ya mtu au kitu). haikusaidii na wala haikufanyi ukaonekana una ujasiri au wewe ni wa kipekee zaidi inaonesha kuwa wewe ni mtu asiyekamilika, una mapungufu na si afya kwako na kwa wanaokuzunguka. Onesha tabia ya hasira inayojenga, na wala si kuwa chanzo cha kuleta utengano, onesha hasira yenye kuleta utangamano kwenye jamii. Tafasiri Unavyoweza

Uwe na weekend njema. Tukutane wakati mwingine tena. Nakupenda Kapuku
Shukrani mtaasisi, leo nimeacha kutafsiri sababu ya weekend [emoji2]

Nyagei
 
...kumbe unayajua na majoka yale basi nimeacha, lol! Unastahili kuingia kwenye kundi la mafundi, ndo maana anko wangu hageuki kila akijidai kujipapatua anarudi, mwanzoni nilidhani ni dawa kumbe roho ndo mwamuzi.

Anko wangu Lyon Lee burudika na hiki kibao

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom