Makapuku Forum

Makapuku Forum

Asante mdau kwa kutupia kumbukumbu hii humu.

Hongera kwa wanawake wote wa Makapuku Forum, nyie ni mashujaa (sheroes) na mnalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo
[emoji122]
 
Tafasiri Unavyoweza: Siku ya Wanawake Wanatangulia Wanaume, Safari Bado Ndefu


Kila jinsi (sex) na siku yake, ipo siku ya wanaume na leo ni siku ya wanawake, wapo kwenye siku yao na siku hii ina historia ya kuvutia kusoma. Ilianza kuadhimishwa nchi za Magharibi na kusambaa zaidi karne ya 20, kuanzia magharibi hakumaanishi Africa, Tanzania kwa mfano na makabila yake hayakuwa yakithamini wanawake na kuwakumbuka kila mwaka kwa sherehe na mambo mengi mengine. Fuatilia jinsi makabila yetu yanavyomchukulia mwanamke na hapa ndipo utajua kuna jambo zuri kujifunza wengine wanafanya nini kuwaenzi wanawake zao na sisi tunafanya nini kuwaenzi wanawake katika jamii etu. Binafsi natoka kwenye kabila ambalo mwanamke ana nafasi kubwa ya kuitengeneza asubuhi yako na kukuletea jioni nzuri ukimheshimu na hata kusalimiana tunasalimiana kwa jina la mwanamke. Tafasiri unavyoweza.

Bado kuna changamoto kubwa sana ya usawa wa kijinsia katika jamii yetu leo, wanawake walio wengi wanaishi kwenye umaskini na utegemezi usio na mfano ukilinganisha na wanaume. Ndiyo, wapo wanawake wenye madaraka makubwa nchini na wengine wanashika nafasi nyeti za maamuzi katika jamii lakini unajua takwimu za sensa zinaonesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume na vipi sasa uwiano kwenye vyombo vikubwa vya maamuzi kama bunge, serikali na mahakama idadi yao ni ndogo sana, tafasiri unavyoweza. Kuna vikwazo vingi wanakumbana navyo kuanzia ndani ya nyumba, kwenye nyumba za ibada, shuleni, makazini na hata serikalini. Tafadhari bila kulali wewe ni mwanamke au mwanaume usiwe kikwazo cha kuifikia safari ya usawa wa kijinsia

Sijamaliza kuandika nikiamini kabisa utamalizia maana nimeandika kama kuchokoza tu mada na kukufanya utafasiri unavyoweza katika kusheherekea siku hii nzuri ya wanawake kimataifa. Ukijitafakarisha ni vipi pamoja na kelele nyingi za usawa wa kijinsia bado kundi kubwa la watu kiidadi linaongoza kwa umaskini, kukosa elimu, utegemezi, kuonewa kisheria na zaidi kunyanyaswa kijinsia. Tafakari na tafasiri unavyoweza.

Hongera wanawake wote mlio Makapuku forum, BlessedHope , Jimena , Shunie , husna muba , ABJ , demi Valentina , Sakayo , Clkey , Tumosa , Linamo , Madame S , na wewe mwanamke ambaye sijakutaja jina lako ila amini tu kuwa wewe unalifanya jukwaa hili kuwa sehemu nzuri sana kuwepo. Hongera na endelea kufurahia siku hii
Ahsante sana mtaasisi
 
Muziki wa Mdhamini: Mama Yangu Ni Mwanamke

...ni bahati iliyoje nikikupa siri ambaye inawezekana ulikuwa huijui. Ninakuambia kwa sababu wewe ni nmtu mzuri na kila wakati unanipa sababu ya mimi kuja hapa makapuku Forum na kufurahia, siri yenyewe ni ndogo sana, niliitunza siku nyingi ila leo nitakuambie na ukiweza katangaze wengine wajue kuwa mama yangu ni mwanamke.

Tufurahie muziki wa mdhamini Sakayo ambaye anataka tufurahi pamoja naye, hakusema anaudedicate kwa nani lakini kwani kuna ubaya kufurahia muziki unaochezwa kwa jirani?

Nitaweka clip mbili za wimbo mmoja, mmoja ni 'original version' na nyingine ni umeimbwa upya 'remix'
Originale






Remix
Hii inaitwa bampa tu bampa
Ahsante mtaasisi kwa good music dedication to our mother's, sister's, nieces, aunt's and all women's in the world.



Leo kwenye weekend music tupigie kibao cha Peter and Andre kiitwacho Mystery girl maalumu kwa makapuku wote.
 
Tafasiri Unavyoweza: Hasira Itusaidie, Isiumize

....nilikuwa nikishangazwa sana na namna kamanda mmoja mstaafu wa jeshi la polisi ambaye kila akiongea alikuwa akionesha hasira hata kama taarifa anayotoa ilikuwa ni ya kuelezea jambo la kawaida sana kwenye nchi za kidemokrasia, maandamano. Hasira ni tabia ambayo kila binadamu anayo, wala usijisikie vibaya kuwa nayo, ila ujisikie vibaya pale hasira uliyonayo inakuwa na lengo la kuumiza, kuua na uharibifu kwa mwingine au vitu (hostile aggression). Hii ni hasira mbaya, haikusaidii wewe wala huyo/hicho unachonuia kukionesha upungufu wako. Tafasiri Unavyoweza

Hasira inaweza kukusaidia, ndiyo pale unapoifanya na kuitumia kufikia lengo jema kabisa kama kutia bidii darasani (instrumental aggresion). Hasira ya kufanya kazi kwa bidii, hasira ya kutimiza ahadi ulizoahidi na hasira ya kuwa mwananchi anayewajibika kwa jamii yake. Muangalie mwanajeshi kwa mfano akiwa vitani kwa lengo la kulinda mipaka ya nchi yake, hii ndo hasira unayopaswa kuwa nayo, mwangalie mwalimu anayeadhibu kwa kufundisha uelewe, jiangalie nawe unapojitahidi kufanya kazi kwa bidii kujipatia maisha yenye furaha.

Usiitumie hasira katili/ovu (hostile) popote pale iwe ni moja kwa moja au kificho (indirect aggression- ambapo unakaa kusambaza uongo na fitna kwa lengo la kuumiza au kuharibu taswira ya mtu au kitu). haikusaidii na wala haikufanyi ukaonekana una ujasiri au wewe ni wa kipekee zaidi inaonesha kuwa wewe ni mtu asiyekamilika, una mapungufu na si afya kwako na kwa wanaokuzunguka. Onesha tabia ya hasira inayojenga, na wala si kuwa chanzo cha kuleta utengano, onesha hasira yenye kuleta utangamano kwenye jamii. Tafasiri Unavyoweza

Uwe na weekend njema. Tukutane wakati mwingine tena. Nakupenda Kapuku
 
Hii inaitwa bampa tu bampa
Ahsante mtaasisi kwa good music dedication to our mother's, sister's, nieces, aunt's and all women's in the world.



Leo kwenye weekend music tupigie kibao cha Peter and Andre kiitwacho Mystery girl maalumu kwa makapuku wote.


Usikonde mtaasisi mwenzangu, nitakirusha muda si mrefu
 
Muziki: Wikend Njema

Ninakusalimia na kukutakia weekend njema kapuku mheshimika. Pole kwa uchovu wa wiki nzima na leo ni furahiday. Jipe raha na nafasi ya kupumzika, usisahau kuwa na wakati angalau wa kunyoosha viungo vya mwili.

Muziki sasa, kwa niaba ya mtaasisi mwenzangu Nyagei tafadhari burudika na kibao hiki na tukutane Jumatatu tena

 
Binamu shikamoo
Halaf kuna siku niliingia humu nikaomba nyimbo hivi hujaona post yangu au vipiii niliomba nyimbo ya tilda ya sweet mother

marhaba aunt yangu
....nadhani ilikuwa ni weekend, kama sikosei jumamosi au jumapili. Weekend napumzika
 
Back
Top Bottom