Muziki: Two In One
.....two in one usifikiri naongelea ule wimbo mzuri wa taarab ya Alhaj Mzee Yusuf, la, hapa namaanisha naunganisha salamu za kukuuliza kuhusu weekend yako ilivyokuwa na kukutakia wiki njema. Upande wangu mambo yalikuwa mazuri sana, nashukuru sana kwa kuendelea kuwa hapa na kulifanya Jukwaa hili kuwa sehemu nzuri kuwepo.
Wiki ya kazi ndo imeanza na kati ya miezi mirefu sana mojawapo ni huu, huwa una wiki tano, sijataka uhesabu kisha ukazikosa unaanza kuniuliza mbona kwaresma imeangukia mwezi huu na easter itakuwa lini, endelea kufunga na kama hujafunga kama anko wangu
Lyon Lee basi angalau funga mlango unapoingia chooni sio kukaa unajikoholeshakoholesha kama umeshikwa na chemba moyo.
Nikushukuru sana
Nyagei mtaasisi kwa kuliweka hai Jukwaa kwa wikend yote na ninarudia tena kutoa taarifa kuwa tangu mwaka umeanza weekends zote hata nikiwepo jukwaani siwezki muziki. Muziki ni siku za kazi tu maana natumia bundle la ofisi.
Muziki sasa, two in one inahusisha kipengele cha muziki na ombi la mtaasisi mwenzangu
Nyagei ambaye ametaka tuburudike na wimbo huu toka kwa mrembo mkongwe le madame Mbilia Bell