Makapuku Forum

Makapuku Forum

Tafasiri Unavyoweza: Matatizo Sio Vikwazo, Ni Miongozo

Hakuna siri kwamba tunapitia mambo mengi sana kibinafsi, kijfamilia, na hata kitaifa. Ndiyo, tunapitia mengi mazuri na mengi mabaya yanayotupa ujasiri, huzuni na mengine yanatufanya tukae chini kujiuliza kama njia tunayoenenda nayo ni sahihi. Njia zote tunazotumia kutaka kwenda tunapotaka si zile zilizonyooka pekee, kuna milima na mabonde bila kuyasahau makorongo na mitelemko. Tafasiri Unanvyoweza.

Wengi wetu ni watumiaji wa barabara, na barabara timamu ina alama za kukuongoza mtumiaji uwe unaitumia kwa miguu au kwa vyombo vya moto. Alama hizi kutaja chache ninazozifahamu ni pundamilia, alama ya kusimama na mwendo sahihi unaohitajika. Ndivyo na maisha yalivyo. Kuna alama za kila namna kwenye maisha na hasa ikiwa wewe ndo ushafikia umri wa kujiendesha mwenyewe. Kujiendesha mwenyewe maana yake kuna wakati utahitaji kuendeshana, tafasiri unavyoweza.

Usikwaze na alama za kukusimamisha (stop signs) hizi zipo, ziheshimu. Matatizo yawe ya mahusiano, kikazi, kifamilia, kiuchumi na kiimani kutaja machache ni alama ambayo haipaswi kukusimamisha katika kile unachoamini ni sahihi kwako na afya ya amani yako. Tumia matatizo kama muongozo (guideline) ya kukufanya ukomae na kulifikia lengo unalohitaji kibinafsi, kifamilia na kitaifa. Matatizo hayataisha na ndiyo maana umepewa kichwa chenye ubongo, yatatue uende mbele unapohitaji. Tafasiri Unavyoweza
Binamu sante
 
....bi Fatma bhana alinikera bora alivyoniacha angenisumbua sana, asante kwa kutumia mbinu zako hadi akaniacha, imekuwa ahueni kwangu.

Ha hahaha, mambo ya booking, hivi kumbe na kwa aunt unafanya booking!! unamaanisha kama si zamu yako kuna mwingine? Mbona mimi nakuwa wa mwisho kufahamu jamani, hebu nihurumieni kesho Ijumaa
Nafanya uchunguzii yakinifuuuu ....make kuna mambo naona siyaelewiii
 
....bi Fatma bhana alinikera bora alivyoniacha angenisumbua sana, asante kwa kutumia mbinu zako hadi akaniacha, imekuwa ahueni kwangu.

Ha hahaha, mambo ya booking, hivi kumbe na kwa aunt unafanya booking!! unamaanisha kama si zamu yako kuna mwingine? Mbona mimi nakuwa wa mwisho kufahamu jamani, hebu nihurumieni kesho Ijumaa
Nimechekaaa [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom