Muziki: Mdhamini Mzungu
..usishangae sana mdau, Kapuku mheshimika, unamkumbuka Shedede, mtu wetu mwenyewe aka
Shadrack K. Lwila ambaye baaaday akununua apple laptop akaanza kuongea kiinglishi utasema muingereza kapoteza paspoti manzese. Alitusumbua humu kana kwamba tusipomuelewa atatupeleka kwa ras Simba kujifunza kubonga ung'eng'e sio kukaa tu kama kereng'enda kujua lugha moja tu kama kifo cha mende. Anko wangu akisoma kifo cha mende basi mawazo machafu yanamjaa anaanza kutafuta maneno ya kiinglishi mara dog style, bad shit heaven (popo kanyea mbingu), big farter , sorry big father na mengine mengi.
Basi mzungu wetu mpya
Mwaipungu kadedicate wimbo wa Changes kwa one of us, the only
makaveli10 muzee ya mapaundi, 'child of cow', mutu ya faranga, makuta, mudogo ya jirani wa dokta Shika. Mabadiliko usipoyakabiri yatakubadilisha na yakikubadilisha kubali kubadilishwa ukijidai kujikaza ukitaka tako utahitaji nguvu ya maandalizi
Tuburudike