"Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.” Mithali 13:3.
Asante Mungu kwa Neno lako asubuhi ya leo, Neno lako linafundisha, Neno lako linaonya na Neno lako linakemea, asante kwa sababu umekuwa ukisema nasi mara nyingi sana kwa kupitia Neno lako, tusamehe pale tulipokaidi kulisikia Neno lako. Mara nyingi midomo yetu imetupoza sana na maneno yanayotoka kinywani hayarudi tena, tumeumiza wengi kwa maneno, tumekatisha wengi tamaa kwa maneno na wengine tumewavunja moyo. Mungu wa mbinguni nifundishe kunyamaza pale nisipostahili kusema neno, naomba useme wewe nisije nikakosea kwa maneno ya kinywa changu nikapata uharibifu.
AMEN