Mungu Baba ktk jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo, ninakisogelea kiti chako cha rehema kwa moyo wa shukurani na taadhima kwa ulinzi ulio tufanyia usiku wa jana na leo hii siku ya Ijumaa, Baba ututakase kwa damu ya ukombozi ya mwanao Yesu Kristo kwa makosa yetu yote tuliyo kukosea kwa mawazo yetu, maneno na matendo.
Baba tunajikabidhi tena pamoja na shughuli zetu, kanisa lako, familia zetu,nchi yetu na watu wote.
Nimeomba haya pamoja na ambayo sijayaomba ktk jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo Aaamin
MBARIKIWE SANA