Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo nitawapa wanawake wenzangu siri 3 muhimu:

1. Maisha ya mwanaume ni kama medani ya vita. Siku zote anajichukulia kuwa yuko vitani. Wakati mwingine analazimika kuficha siri zake kwa sababu anazichukulia kuwa ni siri za vita. Ukiwa msiri atakwambia siri zake, kama huna sifa ya usiri na uwezo wa kuzitunza hatokwambia. Wanaume wengi hawawaambii siri zao kwa sababu wanahisi kuwa siri hizo hazitokuwa salama.

2. Katika maisha ya mwanaume kuna mambo kama 5 humpa wasiwasi muda wote. Katika lugha ya ushauri tunayaita "worries". Miongoni mwa mambo hayo ni UCHUMI wake. Anapokuwa na wasiwasi wa kiuchumi, hujawa na msongo kwa sababu hujihesabu kuwa yeye ndiye muwajibikaji nambari 1 kwa familia yake. Hivyo, wakati fulani kama wamuona mumeo hana raha, ana hasira, kisirani, jazba, ubaridi wa kimahabba, chunguza kama yuko salama KIUCHUMI. Chunguza kama ana deni, mkopo au kitu kingine kinachoendana na UCHUMI.

Na mara nyingi, wanawake wanaopendwa sana ni wale wenye fikra za kumtoa mume kwenye changamoto ya kiuchumi.

3. Mwanaume akiwekewa hapo wanawake wawili: Mmoja akawa anamheshimu, kumsikiliza na kumtii.. Na mwingine akawa anampenda, basi atamchagua huyo wa kwanza. Kwa nini? Kwa sababu hitajio nambari moja ni kuheshimiwa na utiifu.

Hivyo, mwanaume hapendelei kuwa na mwanamke mwenye hisia kali na mhemko uliopitiliza (too emotional), mwanamke mwenye maneno makali, mwanamke anayemponda.

Hizo ni siri tatu ambazo nimependa kushirikiana nawe

Muwe na mchana mwema.
Hii ntaisoma baadae
 
natamani niongezee ila sioni umuhimu,

Umekuwa shunie, wacha tumuite husna tuje kukucheza ngoma..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom