Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Nyongeza ya Mshahara

Ujue nini Kapuku mheshimika, siwzi kuanza kipengele hiki bila kukusalimia wewe unayelifanya Jukwaa hili kuwa la kipekee na la kuvutia zaidi sio kutembelea tu bali kuweka makazi ya kudumu kabisa. Asante na ama baada ya kukusalimia mimi ni mzima wa siha njema (sio lile jimbo la Siha -Moshi, siha = afya) na ninafurahia kuwa hapa kwa sababu wewe upo.

Najua wapo Makapuku wenzetu ambao wamechukua likizo kidogo, na likizo yao maana yake mahudhurio yao hapa yamepungua. Mapumziko ni jambo zuri sana, maana ukirudi unarudi na nguvu kubwa na hii nguvu ndo huifanya KF iwe not a perfect subforum but a great forum to be around. Nyongeza ya mshahara rais kaikataa hata kama wizara ilitangaza kuongeza, sasa najiuliza tu si na yeye atuoneshe paystub zake tone kama hajajiongezea, isijie kuwa tunabanwa sisi tu yeye ndo kwanza hahitaji mkanda tena bali suspender.

Muziki sasa, media nyingi zimetangaza mauaji huko Las Vegas, jiji la maraha, jiji la wacheza kamari na kula bata, na kama yalivyo majimbo mengi hawa bunduki unanunua kama tunavyonunua karanga. Mmoja kati ya wanamuziki ambaye alitumbuiza kwenye tamasha juzi kabla ya yule mbabu kuua watu 50+ ni Jason Aldean, shabiki wa uhuru wa kumiliki bunduki, sasa anajitafakari msimamo wake nadhani anahitaji nyongeza ya mshahara.

Asante kwa muziki Obe Ubarikiwe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom