[emoji524]Zaburi 122
1 Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa BWANA.
2 Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3 Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana,
4 Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za BWANA; Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la BWANA.
5 Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.