Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Ukimya Hauleti Amani

Kapuku mheshimika, u khali gani mdau wa nguvu na wa ukweli kuliko ukweli wenyewe. Naamini uko poa kabisa na maisha yanaendelea na kama Jide alivyowahi kuimba siku hazigandi hata kama zinakwenda polepole. Naamini umekuwa na siku njema sana leo na usiku huu unatafakari yako binafsi yaliyotokea ili upange nini ufanye jua likiwaka tena.

Pamoja na kutafakari yako binafsi ni vizuri kutafakari na ya jamii, hatuwezi kuishi kwa amri ya mtu mmoja au kikundi cha watu, jamii iliyotengemaa inakubaliana na wote, wanaopinga baadhi ya masuala na wanaokubaliana na kila kitu kinachosemwa. Tunajua kukubali (Accept) na kukataa (reject) hakumaanishi mmoja ana mapenzi sana na jamii yake kumzidi mwingine. Sio kweli, anayekubali anaweza kukubali tu kwa sababu kuna masuala yanayomfanya akubali, anakubalishwa kwa nguvu. huyu anaweza asiwe na mapenzi hata kidogo na jamii yake. Anayekataa unaweza kumtaja kama mbaya kumbe ndiye mzalendo wa kweli kwa sababu kwenye kufikia malengo ya jamii anakuja na mbinu mbadala za faida kwa wote (Innovators na retreatism).

Na wanajamii wengine hatari kabisa ni wale wanaoamini kukaa kimya bila kuongea chochote ndani ya jamii ni kuwa salama. Wanaongopa na kujidanganya. simama sema na jamii itakuwa na amani, ukikaa kimya watenda maovu na wabinya demokrasia hawaishii kwa yule peke yake, wakimmaliza watakuja kwako, maana hawatakuwa na wa kumminya tena.

Muziki sasa, endelea kuwa hapa Kapuku Forum kwani uwepo wako unalifanya jukwaa hili kuwa la kipekee kabisa. Ila-liqaa-hadi wakati mwingine

Binamu yangu mm mzee wa samsung galaxy santeee si unajua vile tunakupenda me na anko wako
 
  • Thanks
Reactions: Obe
Usinitenge na uso wako wala roho yako mtakatifu usiniondolee

Unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi

ZABURI 51:11-12

MUWE NA USIKU MWEMA JAMANI DAMU YA YESU IWALINDE MLALE UNONO

NAWAPENDA MIE JAMAN ILA NAMPENDA LEE WANGU ZAIDI BABA D WA KWANGU MIMI SHUNIE
 
Asante aunty yangu. Usiku mwema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom