THE DOM
Sehemu Ya 24
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Instagram....
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
SON OF PRESIDENT GU
Nakupigia magoti sahi, na miguu nakulamba baba nakuomba uwe mchumba wangu kwa dakika tano tu"
Leah aliongea huku akilia machozi, tena wakati huo anaangalia huku na kule Ghafla leah anamuona sauda kabeba jembe lake kichwani,.. Leah akajua sahi akimuona sauda hapa ishu yote itavurugika, na sahi ana hamu na sauda ile mbaya,... Sasa mama sauda nae hamezei jambo,.. Ile sauda anafika tu kwao anapewa taarifa za ujio wa rafiki yake
"rafiki yako leah kaja, yupo kwao sasa hivi... Tena mwenzio kaja na mchumba"
Sauda kusikia hivyo katupa jembe kule, kisha kaanza mbio za kuja nyumbani kwa akina leah, na njia wanayoombana akina sahi na leah ni hio hio anayokuja nayo sauda,.. Ukumbuke sauda nae alisha lala na sahi hivyo sijui patakuaje hapo....
ENDELEA........
Sahi ni mwanaume anaejali hisia za mtu,.. Kweli leah ni changudoa, ila nae ni mwanamke na anastahili kuolewa kama wengine,.. Na hakuna mtu mzuri duniani kama yule anaechukia kazi yenye dhambi au chafu kwa jamii,... Kitu kizuri ni kwamba leah keshaonyesha dhahiri kuacha kazi hio, yaani iwe isiwe ni lazima kuacha,...
Kabla ya sahi kukubali au kukataa kwanza alikumbuka maneno ya mama yake mzazi kipindi hicho kabala ya kwenda korea,...
"mwanangu sheby, natamani sana upate mke mapema mwanangu... Ila baba ndio huyo ni komando anataka nawe uwe komando, yaani sijui itakuwaje mwanangu"
Aliongea mama yake sheby,.. Na hapa ndio tunapata ukweli kuwa huyu sahi ndio sheby aliozaniwa kufariki dunia, sasa mbona sura sio yakwake kama kweli ni yeye,...
"mama, licha ya mimi kufanywa kuwa komando na baba, lakini kuna mwanamke gani wa kuia mama katika dunia hii,... Hakuna mwanamke katika hii dunia, wote ni wachafu hawafai"
Aliongea sahi lakini mama akawa hajamuelewa maana ya maneno yake hivyo mama amesema kuwa
"SHEBY MWANANGU, DUNIANI HAKUNA MWANAMKE MBAYA,.. DUNIANI HAKUNA MWANAMKE MCHAFU,... ILA HAKIKISHA ANAKUPENDA, ATAKULINDA, ANAKUHESHIM, ANAWAHESHIM WAZAZI WAKO, ANAIHESHIM NDOA YAKE,... MWANAMKE KAMA HUYO SIO WA KUACHA,... HATA KAMA WEWE SIO WA KWANZA KWAKE"
Hio ni kumbukumbu ya maneno ya mama yake na sheby ambaye kwa sasa ni sahi,... Sasa sahi baada ya kukumbuka maneni hayo, alimwangalia sana leah huku akitokwa na machozi ili akubalia kuwa mchumba feki mbele ya wazazi wake,..
"Leah,... Sihitaji kuwa mwongo kwako,.. Na sihitaji kuwa mchumba feki,.. Wacha nijitoe sadaka kuoa changudoa... Twende kwa wazazi wako nikawe mchumba wa kweli"
Leah ni kama vile alipatwa na mshtuko wa ghafla, mana alikuwa kimya kwa muda, sio mchezo kitu ulichokipenda kiwe afu kimekuwa vile vile ulivyotaka, sijui utafurahi kias gani, sasa kwa leah ilikuwa ni zaidi ya furaha,.. Alimkumbatia lakini kama vile haitoshi, wakaanza kunyonyana denda, lakini leah akaona kama vile haitoshi
"sahi nikupe nini ili ujue nimefurahi sahi, naomba useme nikupe nini"
Leah alimuuliza sahi ampe nini ili ajue kweli kafurahi kupita maelezo,
"ninachokitaka ni wewe kuiheshim ndoa yako, kuwaheshim wazazi wote, kuniheshim mimi kama mume wako... Ila cha kwanza uiheshim ndoa yako"
"twende baba, hayo yote yamejaa katika moyo wangu,.."
Aliongea leah huku wakikokotana kwenda kwa mama mkwe, na sasa sio utani tena, yaani leah kaokota EMBE DODO kwenye shamba la minazi, ni bahati ilioje kwa mwanamke kama huyu aliojikatia tamaa juu ya kuolewa kwake...
Lakini ile wanaondoka tu, sauda nae huyo,...
"leah jamani mambo"
Ilikuwa ni sauti ya sauda ikimsalimia leah
"heeeee sauda jamani Mambozako"
"safi tu za huko"
"nzuri,... Heee nawe ukiwa kijijini unapendezaga"
"mmmmhhh mwenzangu, nami sina muda narudi mjini mana nimeshapata mchumba mwenzio"
Sasa wakati huo sauda bado hajamuona sahi, yaani sura bado hajaiona mana anajua ni mwanaume mwingine tu, afu istoshe sahi ni mzee wa nguo nyeusi na kofia, hivyo kwa haraka haraka huezi kumuona...
"weee sauda acha utani"
"ndio, na keshantumia nauli yaani ni mimi kwenda tu"
"ok, basi shem lako ilo apo"
Leah alimtambulisha sauda, wakati huo sahi anafurahi sana kwa kumuona mtu wake.. Sasa ile sauda anamwangalia vizuri, mbona ni yule askari aliomwibia ile dom,... Ila sauda hajui kama ile inaitwa dom na hajui kazi yake, yeye aliiba tu,...
"za saa hizi shem"
"salama tu hali yako"
"safi tu"
Sauda aliogopa sana mana anamjua
"aahhh nadhani unanikumbuka vizuri eee"
Aliongea sahi huku akimshika bega
"ndio"
"tafadhali sana, sikuhitaji wewe, wala sihitachi chochote toka kwako, ispokuwa kile kifaa tu,.. Ulikiuzia wapi tukakikomboe"
Aliingea sahi, wakati huo sauda anatetemeka, mana anamjua huyo ni askari,.... Sauda hajui ajibu nini, hajui atamwambia nini... Lakini alishaona kuwa kitu anachokitaka sahi kinaonekana ni cha gharama kubwa sana, hivyo wacha amchombeze kwanza
"honey, naomba twende kwa wazazi kwanza,.. Wanatusubiria pale nje"
Aliongea leah huku sahi akimsikiliza leaha kama mkewe mtarajiwa,..
"sauda, kama hukumbuki, nakupa robo saa tu, ukumbuke hilo suala"
Sahi aliongea hivyo kisha akaelekea kwa wakwe zake,...
Sauda anarudi kwao, hata hamu hana, kaiba kitu sasa leo kaletwa na kajulikana mpaka anapoishi
"umemuona rafiki yako"
"ndio mama..... Ila kuna kitu niliibaga mama, na huyu kaka ndio kanifuata mimi"
"uliiba??... Uliiba nini"
"mimi hata sikujui hicho kidude... Na nilikitupa kule kule Dar es Salaam"
"mungu wangu sauda wewe, yaani najuta kukuruhusu uende mjini mwanangu"
Aliongea mama yake sauda huku nae akitamani hata kulia
"mama, afu mbaya zaidi huyu mwanaume mi askari"
"uuuuuuwiiiiiiiiiii, yaani mapaka hapo siko na wewe tena"
Aliongea mama sauda huku akilia sana,....
"mama, sina budi kumpeleka nilipokitupa"
"mungu wangu mwanagu huenda usirudi tena sauda"
"mama, nisamehe sana mama angu"
Huku kwa akina leah na sahi, ndio wanamalizia Malizia kubarikiwa uchumba wao na wazazi wa leah....
"leah mwanangu, sasa umeshakua mchumba wa mtu, utulie mwanangu"
Aliongea mama kumwambia mtoto wake, na wakati huo sahi yupo na mzee ambae ni baba yake leah,.. Yaani mwanaume kwa mwanaume na mwanamke kwa mwanamke... Kwahio kila mmoja anamshauri kijana wa jinsia yake,..
"mama, hilo ninalo kichwani,.. Siwezi kumdharau mume wangu, siku zote nitakuwa chini yake"
"halafu kingine ni kwamba,.. Mwanamke hanaga dini, huyu kijana ni Muislamu na sisi ni wakristo,.. Ni lazima uende upande wake"
"mamaaaaa.... Hilo kwangu ni jambo rahisi sana,.. Kubadili dini kwa ajili ya mume wangu, nipo tayari mama"
"basi lazima ndoa yako idumu mwanangu"
"afu mama, tuna haraka sana eti tunataka kuwahi mambo ya mjini, mana si unajua kazi kazi hizi"
"ni kweli mwanangu, basi mimi nawatakia Safari njema.... Ila saa hizi mtapanda basi gani jamani"
"mama, tumekuja na usafiri wetu"
Aliongea leah huku akimfuata sahi kule kwa baba yake mkwe,.. Mana alikuwa anaongea na mwanaume mwenzie
"kijana wangu, mimi nadhani wewe ndio unaanza kuingia katika ndoa... Kitu kikubwa cha kuzingatia... Mwanamke ni kama ua, mmoja wenu akiwa chini basi ndoa yenu itadumu sana, hivyo jitahidini sana mnapokwazana mmoja ajishushe kikauli"
"sawa sawa mzee wangu"
"ila sio wewe.... Wewe hutakiwi kushuka sana kijana,... Wanawake wa siku hizi ukijishusha tu, nae anapanda kichwani, hivyo kuwa makini sana kijana, Mana sasa umeshakuwa mkwe wangu"
Baba yake leah alikuwa akimpa sahi lisala juu ya kuishi na mwanamke,...
Basi leah alifika pale na kuaga kwa baba yake,... Ila walipo piga hatua kama mbili hivi lea alimwomba sahi pesa kidogo
"sahi mme wangu,.. Hapa nina elfu 15 tu hii hapa... Natamani niwaachie wazazi kiasi kidogo, lakini sasa haitoshi mme wangu"
Aliongea leah tena kwa upoleee, mana keshafundwa na mama yake huko kuwa mume hahitaji sauti ya juu hata siku moja... Basi sahi alitoa waleti na kutoa kiasi cha laki mbili,
"wape hii, hio yako achana nayo"
Leah alirudi nyuma na kuwapa wazazi wake ile pesa aliopewa na sahi...
Basi wazazi ni furaha gani hio, na hio ndio faida ya kuwa na mtoto wa kike,
Wakati huo huku sauda keshajiandaa mana swala la kurudi mjini lilikuwa na ulazima ila sio ombi, yaani ni lazima arudi mjini kuonyesha kifaa cha watu,.. Kwani palikuwa na cha kusubiri,.. Walitoaka hapo mpaka walipoacha gari yao, mama sauda anajua mtoto wake kurudi ni ndoto tu
Kwa jinsi sahi anavyoitamani kuipata dom, yaani hataki mchezo kabisa.... Basi safari ya kuja mjini jijini Dar es Salaam ilianza, na uzuri ni kwamba ilikuwa ni mapema sana,..... Sauda hana raha kabisa yani, mana ni wiki mbili zimeshapita toka akitupe kifaa kile,... Sasa je? Watakiona.....
Sasa huku jijini Dar es Salaam, nyumbani kwa Mheshimiwa rais,.. Mzee akiwa sebuleni anaangalia tv, alishangaa kusikia sauti ya kilio huko chumbani kwake,.. Akatilia mashaka hurnda ni mke wake,... Na ni kweli alikuwa ni mke wake aliokuwa akilia
"we vipi tena, chato kuna msiba"
Aliuliza mr GU huku akimuamsha mkewe,...
"siamini kama mtoto ndie aliekufa"
Aliongea mke wa rais huku raisi akishangaa kwa maneno ya mkewe,..
"huyu mtoto sintomuua bi ni lazima nimtumbue, mi nikajua unamlilia mtoto nani kumbe ni huyu fara... Lazima nimtumbue jipu, afu na vile kakataa wito wangu.. Yaani sipati picha"
Aliongea mzee GU huku akiondoka chumbani taratibu..
"mimi simsemei Joseph"
Aliongea mke wa rais huku rais akigeuka kwa mshangao na kuuliza
"unamsemea mtoto gani, na sisi tuna mmoja tu"
Sasa mama kabla ya kumwambia mumewe, kwanza alikumbuka siku ya jana wakiwa kwenye semina ya akina mama....
Wakati semina hio inaisha na mgeni rasmi alikuwa ni mke wa raisi,.. Lakini ile mke wa rais anaingia tu ndani ya gari, kuna mama mmoja hivi akamuita...
"mwanangu, mwanangu samahani sana"
"bila Samahani mama shkamoo"
"marahaba... Mwanangu kama nakukumbuka"
Aliongea mama huyo wa makamo sana tu,
"mmmhhh labda, ila mimi sikukumbuki"
Aliongea mke wa rais huku akiwa na shauku ya kukumbushwa
"miaka kadhaa ya nyuma, mimi nilikuwa ni dokta,.. Nakumbuka mlikuja kujifungua katika hospitali moja, mlikuwa wanawake wawili afu wote waume zenu ni wanajeshi"
Sasa mama Joseph au mke wa rais akakumbuka ni kweli
"waoooo wewe ndie yule dokta ulietuseidia"
"haswaa.. Ilikuwa ni zamani sana... Halafu waume zenu wajinga sana yaani wanakuja kufanyia mazoezi hospitalini"
Aliongea mama, mana kipindi hicho rais GU na General Nyange walikuwa ni marafiki wakubwa sana, walisoma wote, wakajiunga na jeshi wote, kwa furaha hata ndoa zao zilifungwa siku moja... Kizuri zaidi hata wake zao wote wakashika ujauzito kwa wakati mmoja,... Ila siku ya kujifungua, alianza huyu mke wa rais, sasa mke wa General ndie alikuwa karibu sana na mke wa rais, hivyo alivyosikia mwanamke mwenzie atajifungua kwa operesheni,.. Mke wa General alishtuka na kuanza kuskia uchungu ghafla, lakini yeye hakuwa wa siku hio ila kwa mshtuko, ikawa siku hio hio na wakajifungua siku mbili tofauti, yaani walifuatana... Sasa vitoto vyao vikawa vimelazwa katika kitanda kimoja.... Sasa kumbe majamaa akataka kuwakaribisha watoto wao kijeshi jeshi.. Saa ngapi wasije na mabunduki hospitalini,.. Mlinzi kuona mabunduki, akatangaza vita imeanza, basi viashiria hatari vikawashwa, ili mwenye kujiseidia ajisaidie.. Sasa wale wazazi wawili wakakurupuka na watoto wao... Kumbe wakati wanachukuwa watoto wao, walijichanganya na kila mmoja kuchukuwa mtoto wa mwenzie... Na hivyo ndivyo ilivyokuwa...
"hahahahaha bwana mama unanichekesha sana... Unajua wao walikuwa wanajeshi kweli, na walitaka kuwakaribisha watoto wao kijeshi jeshi na ndio mana wakaja wanajeshi wengi pale hospitalini"
"sasa kama unakumbuka siku ile mlikuwa watu wawili mlijifungua chumba kimoja na yule mwenzio yule unamjua... Lakini wakati ile vita inatokea, wewe ulichukuwa mtoto wa rafiki yako,.. Nikatamani kukuambia lakini nikaikosa nafasi"
"ati unasemaje??... Yaani nilichukuwa mtoto wa rafiki yangu"
"ndio... Mimi nakumbuka wewe ndio wa kwanza kujifungua,.. Na mtoto wako ana alama hapa chini ya jicho la kushoto"
Sasa mke wa raisi ndio anakumbuka mtoto mwenye alama ni yule mtoto wa General nyange ambaye ndio sheby, au sahi wa sasa hivi, lakini mke wa raisi anajua kuwa yule mtoto alikufaga...
"we mama acha utani"
"mimi nakuambia sasa, ulichukuwa mtoto wa rafiki yako.. Umelea mtoto sio wako"
Pale pale mke wa rais akaanza kulia, lakini mama akamuuliza
"unalia nini sasa, yaani kukupa ukweli ndio ulie"
"hapana... Nalia kwasababu huyo mtoto keshafariki dunia.."
"ooohhh pole sana"
Kumbukumbu ya mke wa rais baada ya semina iliishia hapo...
"baba Joseph, kumbe yule kijana ni mtoto wetu"
"kijana gani huyo"
Hata mheshimiwa GU hajui kama sahi ndio mtoto wake,.. Yaani Joseph ndio mtoto wa Generali nyange, sema haijulikani....
"yule mtoto wa rafiki yako"
"unasemaje"
"ndio.. Jana nilikutana na dokta akanipa ukweli wote, na sababu ni ule ujinga wenu wa kuja na mabunduki hospitalini, mpaka watu wakachanganyikiwa"
"ahahahahahahahahahaha saaafi sanaaaa"
"sasa unacheka nini baba Joseph"
"hahahahahaha kama ni hivyo basi safi sana... Huyu sahi unaemuona anakuja kuja hapa ndani... Ndio yeye huyo.. Hahahahahaha saaafi sana"
Mzee GU alifurahi sana kwa taarifa hizo, mana amepata kijana shujaa
"unasemaje baba Joseph"
"weee koma, mimi sio baba Joseph wewe"
"heeeee mara hii umeshamkana mtoto uliomlea"
"sina mtoto jambazi mimi"
Baada ya siku hio kupita, kesho yake sahi na sauda wakiwa katika dampo, yaani sahi haamini kama dom imetupwa dampo, yaani haamini macho yake Kiukweli...
"yaani sauda unatupa kifaa kama kile dampo?"
Aliongea sahi huku akitamani hata kulia, lakini sasa mbaya zaidi taka taka zilishachukuliwa na kwenda kumwagwa dampo kuu.. Hivyo hapo ni peupeeeee....
Sahi alikimbia manispaa ya jiji hilo na kupewa mamlaka ya uongozi wa mtaa ule,...
"takataka zilichukuliwa jana"
"tafadhali sana ndugu, naweza kujua aina ya gari inayochukua takataka hapa"
"ndio.. Na dereva yupo ndani"
Mara moja kumfuata dereva, kaongea nae sana kuwa takataka alizochukuwa upande huu, alizitupa upande gani kule dampo kuu... Dereva akawa anasita kuingea, sahi kavuta waleti katoa laki Mbili
"haya niambie"
Wakati huo wapo dampo kuu hapo
"nilizimwaga pale, na ni jana tu"
Sahi alipo onyeshwa tu hajapoteza muda, si unajua dampo kuna wale watoto wa mtaani wale,... Akawaita na kuwaonyesha kitu watakachokitafuta... Jamani pesa inaweza kufanya lolote lile,.... Sasa sahi anaona wanachelewa kutafuta, nae akaingia kwenye kazi, sahi alivaa nguo zake nyeusi safiii,... Alichafuka hata kichaa ana nafuu, lakini mungu sio asumani kweli DOM hio hapo keshaiona, haamini macho yake kama kweli kaiona dom, yaani alichokifanya ni kuibusu hata kama ilikuwa chafu,... Aliwalipa wale watoto pesa nzuri sana... Sasa ile anaondoka na furaha zake, mara simu mbili zinaita, simu ya mkononi na simu ya sikioni,... Ila simu ya sikioni ananua nani anaepiga ila simu ya mkononi hajui nani anapiga.. Kwanza aliipokea simu ya sikioni ambayo ni ya mr GU,...
"hello"
"Mjerumani amekuja anataka dom, sasa sijui upo wapi sasa hivi"
"nakuja nayo sasa hivi mzee"
"harakisha"
Sahi aliachana na ile simu, na hua haikatagi hio simu, sasa baada ya kuongea na hio simu ya siri, sasa katoa simu ya mkononi... Lakini alishangaa jina liliopiga....
"MAMA"
aliongea sahi huku akitabasamu kwa kuona simu ya mama yake, wakati huo kachafuka, ananuka kila kona ya mwili wake...
"hallo mama yangu mzazi shkamoo"
Aliipokea kwa furaha kubwa sana lakini ghafla anasikia
"sheby mwanangu, usije huku na usilete hicho kitu wanachokitaka... Baba yako kaniteka huku ananitesa sana... Usije tafadhali sana baba"
Ilikuwa ni sauti ya mama yake,.. Lakini ukweli wa mama wa sahi ni mke wa rais GU, hivyo huyu ndio ndio mama wa Joseph...
Mara ghafla sauti ikabadilika
"kama unampenda mama yako, utaileta hio dom,.. Nadhani unanijua mimi baba yako, siangalii huyu ni mke wangu au laaa,... Naua kama usipoleta hio dom hapa... "
Aliongea general Nyange lakini kwa mbali sahi akasikia sauti ya mama yake ikisema
"mwanangu usijeeeeee, acha nife tu"
Je? Sahi atakubali mama yake afe?? Na je? Wapi ataipeleka dom???...
ITAENDELEA.....