Makapuku Forum

Makapuku Forum

Jumamosi Fleva: Jipende Mwenyewe

Ni Jumamosi nyingine tunakutana kwenye muziki na kama kawaida maneno machache muziki unatawala. Hapa KF leo ni muziki wa kileo zaidi na si ule muziki wa wahenga. Ila ujue nini, hata hawa vijana wa leo wanaoniita muhenga jioni hii asubuhi ikifika nao wataitwa wahenga. Maisha ni mzunguko.

Jipende mwenyewe maana ni wewe mwenyewe ndo unajijua, wengine hutoa complimentary tu ila ikifikia kujipenda, jipende mwenyewe kwanza na mengine yatakuja tu. Sisemi kupenda au kupendwa sio muhimu, namaanisha ukijipenda mwenyewe na mwingine atakupenda, usipojikubali hakuna atakayekukubali.

Asante kwa Shunie aunt yangu wewe kwa kuchukua nafasi ya kutupatia sala na maneno ya hekima, unafanya vizuri sana na ninakupenda kama unavyopendwa na wengi. Unalijua hilo, tabasamu maana ndivyo unavyonifanya nitabasamu. Asante sana.

Tuburudike sasa na kwa usiku huu tumwangalie Justin Bieber- Love Yourself (nimesikiza dirty version yake huihitaji hapa) akiperfom live huko Manchester kwenye Tamasha la One maalum kuchangia shirika la Msalaba Mwekundu.


Asante binamu yangu nakupenda sana unajua hilo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom