Makapi ya mafuta si misingi ya Taifa

Makapi ya mafuta si misingi ya Taifa

Alloyce PR

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2020
Posts
590
Reaction score
706
"Vijana wa kizazi cha leo wanaamini afya iko kwenye mafuta; mihogo ya kuchemsha ni ya washamba, lakini ya kukaanga ni fasheni. Dagaa ni za maskini, lakini kuku wa kisasa anayewanenepeesha hadi wanaume kuwa na matiti kama wake zao ni starehe kwao. Halafu unategemea kupata taifa lenye vijana wenye akili iliyokomaa? La hasha! Utavuna makapi ya mafuta yaliyojaa ladha, lakini hayana maarifa, kazi kwao ni kutukana, na kulalamika." —Alloyce, P.R. 🥴💭
 
Maisha ni mafupi uncle acha watu waishi maisha yao.

Upate Nyama ya kuku mzima, ugali kidogo, pilipili pembeni ,na soda ya pepsi pembeni aaaaah weee Acha kaka
 
Maisha ni mafupi uncle acha watu waishi maisha yao.

Upate Nyama ya kuku mzima, ugali kidogo, pilipili pembeni ,na soda ya pepsi pembeni aaaaah weee Acha kaka
😂😂😂 nimekuelewa mkuu.
 
Inategemea njia zilizotumika kuwaandaa. Wamendaliwa waje kufikiri na kutenda kwa namna gani.
Kila kitu ni matokeo ya mchakato wa inputs, process, time na mazingira. Kuwalaumu wao naamini kwa kiasi kikubwa sio sahihi sana.
 
Back
Top Bottom